Dashboard Builder for Access 2.0 Antivirus Report

Wednesday, December 29, 2010

Saikolojia ya rangi

AINA MBALIMBALI  ZA RANGI YA MAVAZI UNATAKIWA UVAE  MAHALI NA KATKA SHUGHULI TOFAUTI:
Saikolojia ya rangi inachukua nafasi kubwa sana katika maana ya mambo(saikolojia)hapa duniani,rangi inachukua nafasi ya kukutabiria wewe nini unataka kiwe ili ufanikiwe au la,haijalishi ka kama wewe umepangalia rangi au hukupangalia(imetoke kwa kutokujua)maumbile ya dunia yapo kukupatia kile ulichoomba(request)na sio vingine kwa lugha rahisi dunia ina kanuni na inabidi uwe ndani ya hizo kanuni ili ufanikiwe,dunia inakupatia mafanikio  au la,nimeshuhudia mara nyingi watu wengi wanashindwa kufanikiwa katika mambo mbalimbali kwa kuwa nje ya kanuni  na ndoo hii sababu ya kuandika makala hili,dunia ina rangi kuu zifuatazo nyeupe,nyekundu,bluu,njano,green,kutokea hapa rangi nzote nyingine zinatoke hapa kwa mchanyiko wa hizo hapo rangi mfano pink,majivu nakadhalika,mara nyingi inashauriwa kuvaa rangi hizo kuu maana zinatoka ujumbe kamili,kila rangi ina maana kubwa kwenye haya maumbile ya dunia,maumbile ya dunia yanafuata kanuni na yatakupatiakile unakihitaji kulingana na lugha yako.Zifuatazo ni aina za rangi na matumizi yake mahala tofauti na shughuli tofauti,
1.Nyekundu,ni rangi  inayotumika katika kutoa amri(order)au ni ya kiutawala zaidi huwa inaamanisha amri  na lazima jambo Fulani lifanyike ,huvaliwa  na mtu mweye cheo kikubwa zaidi wengine kuwaamurisha wenzake mfano maofisini bosi anapotaka anapotaka jambo au kazi Fulani imalizike kwa muda Fulani siku hiyo huvalia tai yake ya nyekundu na katika kikao utaona jinsi anavyo toa amri watu wanatii na kuogopa,Pia maraisi wa nchi hutumia nyekundu pale wanapoenda kutoa amri au kushinikiza jambo Fulani hii inaweza kwa viongozi wenzake mfano mawaziri,hata wananchi nakweli utaona utekelezaji wa jambo hilo kiurahisi,Nyekundu pia hutumika katika mabadilishano ya kibiashara(negotiation)mfano mwaka huu Barack Obama na  raisi wa Urusi Drimitry Medved walipokuwa pale marekani kufanya maongezi ya kibiasha kati ya nchi zao  Obama alivaa tai nyekundu (alikuwa na sauti kubwa maana yake) na raisi  wa Urusi alivaa blue (aonewe huruma)hii ilikuwa mawasiliano tosha tuu na hawakuvaa kibahati ilikuwa impangiliwa hivyo.
2.Bluu(blue),hii ni rangi ya ulizi(protection)hii ni rangi muhimu sana yaw ewe uonewe huruma na watu wengine,mathalani hutumiwa kwenda kuomba kazi kwa kampuni mbalimbali ni vema ukavaa tai ya blue kipindi cha interview wale wanaokufanyia usahili hata kama utakuwa unaukosefu wa jambo Fulani lazima wakuonee huruma na kuweza wewe kupita,Blue pia huvaliwa kipindi cha ujenzi na mafundi ndoo maana overall la kwanza kabisa lilikuwa la rangi ya blue ikiwa na maana ya ulizi(protection).Blue pia hutumika kipindi cha wewe kusafiri kwenda sehemu mbalimbali unasafiri  vaa blue kuanzia nguo ya ndani   hapa utakuwa una ulizi kamili.Katika majadiliano ya biashara au mengine kama wewe huna nguvu(sauti katika hayo)vaa blue huruma itawajia wale unaofanya nao mazungumzo na hivyo kuto nyonywa

3.Njano,hii ni rangi ya umakini hii hutumika kama unataka watu waweke umakini kukusikiliza wewe na kuelewa kile unachokisema  sana sana kwenye hotuba,mahubiri,semina,mikutano nk ni rangi husika kuvuta umakini kutoka kwa watu,vile vile njano hutumika katika kusoma,au kuwa busy juu jambo Fulani hivyo kuonyeshea wengine kuwa wewe upo katika hali ya kutotaka usumbufu wa aina yeyote ile na hivyo  kukuacha na umakini wako,mfano ukiwa unasoma unashauriwa kama hutaki usumbufu kutoka kwa wengine vaa njao utaona jinsi utakavo kuwa huru.
4.Green,ni rangi muhimu sana inayomaanisha kuzidi kukua na kuimarika mfano kampuni au jambo Fulani.Green ni rangi ya mimea  na mimea imeenea kote ulimwenguni hivyo green katika maumbile ya dunia inamaana ya kusambaa au kukua na kuimarika mfano pale kampuni inapotaka  kukua kwa kasi na kusonga mbele kwa kasi utakuta  wafanyakazi wamevalia t-shirt green hapa kuna maana kubwa sana kwa maumbile ya dunia,Kenya ilipopitisha na kuanza kuyatekeleza maono(vision)2030 iliweka rangi ya green  hii ilikuwa na maana kubwa sana katika maumbile ya dunia kuwa Kenya inazidi kukua na kusonga mbelembele  hii rangi Kenya haikuweka kibahati ni plan ya wao kuendelea.


5.Nyeupe,ni uwepo wa rangi zote hutokana,nyeupe hutumika katika maeneo ya ibada,sherehe za amani na furaha,nini nyeupe ina maani kwa maumbile ya dunia?nyeupe inaonyesha usafi wa mtu rohoni,utayari wa kusaidia watu wengine,amani ya mtu kwa watu,yaani mambo yapo
salama,pendelea kuvaa nyeupe wakati wa ibada za kufunga,meditation,sherehe za kusaidiaa watu wenye shida,sherehe  na matukioyanayo maanisha amani
Wengi nazani mtajiuliza je nyeusi je?nyeusi ni kutokuwepo kw rangi yeyote,hivyo nyeusi si rangi,katika maumbile ya dunia huja yaambia jambololote lile hivyo lolote lile linaweza kukuadhiri wewe kwa sababu haupo kwa rangi yeyote,
Mchanyiko wa hizo rangi hapo juu ndoo tuna pata rangi nyingine chungu nzima mfano pink hutumika wakatik machombezo na mpenzi wako,ukiwa upo ndani pink ni rangi ya mahaba na ni nzuri wapenzi wakiivalia wakiwa katika stori za mahaba.
Matuki na aina za rangi
Interview-blue
Kusafiri-blue
Kutoa amri-nyekundu
Msibani-blue
Kuhutubia/kufundisha-njano
Kukua na kuimarika-green
Kusaidia jamii-nyeupe
Kutaka watu wakukubali-blue
Tumia rangi sasa ikupatie  ikupatie mahitaji yako,lolote tukio utakalo lifanya litende kwa umakini na uhakika sio tu kufanya mambo kwa kubahatisha na mwishoe kuwa mtu wa ajabu
Ukitaka kuendele mafanikio yapo mikononi mwako amua leo.

2 comments:

THIS IS YOUR PLACE TO COMMENT