Dashboard Builder for Access 2.0 Antivirus Report

Saturday, December 4, 2010

MICHAEL....

d                        KUWA MSHINDI KATIKA KULALA VEMA:  
Baada ya kazi na miangaiko mingi ya siku  mara ofisini,nyumbani na sehemu nyingine  mchoko kama huu wote huishia kitandani lakini mara nyingi watu wengi huwa wanalalamika  mara usingizi sipati ,hata muda mwingine wengine hupata usingizi asubuhi  hili tatizo limekuwa kubwa siku hadi siku ndani ya jamii zetu, kitaalamu tatizo la kukosa usingizi huitwa insomnia ,na mara nyingi wengi wanaokumbwa na tatizo hili wamekuwa wakijaribu kutafuta suluhu mbalimbali mathalani wengi  wanajaribu  kutumia madawa ili tu waweze kulitibu tatizo lakini mara zote hii inakuwa suluhu ya muda mfupi tu,siku moja nilikuwa na dada mmoja  alikuwa ananilalamikia kuwa yeye hapati usingizi nahivi sasa yapata miezi sita.kweli ilinigusa sana  na pia aliniambia amejaribu kutumia madawa lakini hayakufua dau kweli hii ni kama kifungo mtu yupo nilimapatia ushauri na baadanya muda aliniambia tatizo limekwisha,katika tafiti mbalimbali mathalani kutoka university of Harvard medical school wanasema kulala ni muhimu sana kwa afya ya mwanadamu muda wakawaida wa mwanadamu kulala kwa usingizi wa afya njema ni masaa manane,utafiti unaonyesha kuwa watu wanaolala kupitiliza masaa nane   mfano wanaolal masaa tisa,kumi nakathalika  huwa wanajitafutia matatizo,inasemekana watu  hawa  kiwango cha waokuishi ni kidogo sana maana ni rahisi kushambuliwa na magonjwa ya moyo mfano heart stroke na mengine  kuliko watu wanaolala masaa ya kawaida nane,miongoni mwa wanaolala masaa tisa kiwango cha kufa ni asilimia286 juu zaidi ya wanaolala masaa saba,vilevile wanaolala masaa chini ya nane mfano matano hukumbwa na matatizo kama kuhisi maumivu kutwa nzima,kutojisikia vema (discomfort) na kwa ujumula  huishia kuthoofika kiafy.
Kuna jinsi yakufanya ili uweze kupata usingi murua na mzuri ,tafiti zinaonyesha mambo yafuatayo yanaweza kukusaidia kuwa na usingizi mzuri kabla ya kwenda kitandani:
 i)Penda fanya mazoezi mepesi kabla ya kwenda kulala,mathalani kunyoosha viungo,puishapu kadhaa
ii)Oga na maji ya vuguvugu  kabla ya kwenda kulala nyakati za usiku.
iii)Sikiliza mziki taratibu na wenye kukuliwaza,ni muhimu sana kununua cd za muziki wa taratibu wakati wa usiku unaiweka na kusikiliza
iv)usipende kwenda kulala wakati huohuo umetoka kula chakula,usipende kuingia kitandani na tumbo lililojaa chakula havita kuletea usingizi
v)Matatizo  yako ya siku nzima usiende nayo kitandani
vi)Kaa katika mawazo mazuri,furaha,amani ya moyo
vii)jiachie mwili wako,akili yako,weka hisia wewe ni mwepesi,weka fikra kuwa usingizi unakuja na jiweke katika mazingira ya kuukubali usingizi

salamu za Kilawe

KUONGEA SANA  INAWEZA KUKUSABABISHIA WEWE UKOSE  FURSA ZA NAFASI NA MAARIFA KUTOKA KWA WENGINE:
Binadamu ameumbwa  na macho mawili,masikio mawili hii ni viungo muhimu sana katika kumpatia mwanadamu taarifa kutoka kwa wengine,mdomo ni mmoja tu kapatiwa na kutufanya sisi  kutoa taarifa kwa wengine,kwa mantiki ya kawaida hii inamaanisha kuwa wewe  unatakiwa kupokea mara mbili  zaidi ya kile unachokitoa kwa wengine,nahii haina ubishi na haijalishi wewe ni nani au unafanya nini hii ndio sheria iliyo toka enzi na enzi kuanzia china ,ulaya,Afrika na kote duniani wengi watoaji taarifa za kutoka kwao kuliko kupoke huishia kuwa wepesi wa mwili,fikra na kukosa kujiamini kwa mambo yao kwa kuwa hawana jipya au jambo wengine hawalifaamu na kuishia kuwa watu wa kawaida sana na kuwanufaisha wenzao kukua,utaweza jiuliza sana kama ndoo hivyo kwa nini mtu kama mwanasiasa au mchungaji au shehe wanawahuburia sana watu wao lakini kila siku bado wapo imara sana ,sheria ipo pale pale hapa sio kama hawapati taarifa kutoka kwa wengine huwa wanapata sana mfano kupitia kusoma biblia,quruani, novel na vitabu vingine,pia,meditation, kuangalia movies,taarifa za habari hivi  vyote ni vyanzo vya kupata taarifa
Katika maisha  ya kila siku nimeshuhudia  vilio mbalimbali kutoka kwa watu wakijilaumu  na kusema wao si chochote hapa duniani na kweli wenzao hawawathamini  na kamavile wametengwa pasipo  maagano rasmi ya kutopokea taarifa muhimu kutoka kwa wengine,lakini ukiangalia chanzo  cha tatitizo linatokana na wao kuongea sana na kusababisha wao kufukuza maarifa kutoka kwa wengine na taarifa nyingine muhimu .Dunia  hii ndugu imeumbwa na kanuni na jinsi ya kuishi inabidi tutumie kanuni kwa yeyote Yule anayeenda kinyume na kanuni hizi  lazima aangalie wapi alipokosea na arudi nyuma ili asahihishe kosa anza sasa kuwa mjanja kataa taarifa zako kila mtu akazijua hata kama ni mkeo,mzazi au ndugu yako shirikiana nao lakini sio kwa kila taarifa uliyokuwa nao namaanisha kuwa na siri au” msiri” ,binadamu aliyekosa usiri anamatitizo Fulani maana hata mungu ni msiri sana ili shetani kwa wale wanaomaamini asimpiku jaribu kupokea  kutokakwa  zaidi au soma vitabu sasa,
Njia nyingine ya kutokuwa mzungumzaji sana ni kupenda kuyachukulia mazungumzo  yako ni ya kawaida na sio ya ushindani kwa wengine lengo ni kufikia muafaka. Tatu,unapoona mtu anazungumza acha kumkatisha msubirie mpaka atakapo maliza,na hata kama ataongea sana itafika wakati yeye atatambua wewe pia unahitaji kuongea, hakuna mtu mkamilifua jua hilo.
Mara zote huwa nasema huwa tunafukuza ndoto za kufanikiwa pale  tunapochukua muda wetu kuongea sana kwa kupitiliza anzan sasa kutafuta taarifa muhimu kuliko kutoa ovyo ovyo taarifa  soma  sana vitabu humo ndiko kuna taarifa muhimu,udhuria mikutano muhimu,soma magazine mbalimbali kama fobres magazine kweli utafanikiwa mafanikio ni kwa wote maana dunia  ni yangu na wewe na wengine wote.

Thursday, December 2, 2010

Kilawe Deogratius mjasiriamali aliyebobea aanziasha new project.........

Baada ya kufanikisha project yake ya  stationary  bab kubwa na lenye kutoa huduma kwa bei nafuu,mjasiriamali na mwandishi wa makala za kuchochea kufanikiwa Tanzania,sasa ameanzisha project yake ya  kuwafundisha watu jinsi ya kutengeneza blogspot kwa bei  ndogo sana  ambayo mtanzania anayeishi chini ya dollar mioja anaweza kuimudumu hii nia idea ambayo Mr Deogratius kilawe analengo la kila Mtanzania kuwa na yake blogspot ,...........,vilevile Mr Deogratius Kilawe  amefungua rasmi  project kabambabe ya kutengeneza website nzuri zenye hadhii ya kimataifa na mishiko kwa watu wote  kwa kampuni za kitanzania  na nje ya kitanzania kwa bei nafuu..... kwa mawasiliano na Deo kilawe unaweza mpata kwa  0717109362 au email:deogratiuskilawe@yahoo.com

How do I put AdSense on my blog (using a classic template)?

kupitia hapa unaweza kutengeneza fedha na google

makala la kwanza.

TUNAISHI KWA KUTEGEMEANA ACHA VITA
Dunia sasa imegeuka kijiji ,utandawazi ndoo sera inayoendesha ulimwengu ,mikono yake ipo
kila mahali uanpokuwa ukiwa nje ya kanuni za utandawazi itachukua muda wewe kuendelea,soko
huruia ndoo inaangaza dunia zima kuanzia USA,UK,Tanzania mpaka China na kote duniani,kila mtu
anapigania kuwa na mtandao wa marafiki,business partners wengi kwa wingi pasipo kikomo,wengi
wanapigania kujifunza tamaduni za wengine kwa kasi ili waweze kusurvive katika hii dunia maana
ndoo sera inavyosema.Je ulisha wahi kujiuliza siku ukianzisha au vita unayo sasa kupigana au
kutoelewana na wezako huoni ni kizingiti ndugu yangu,kuna watu wengu katika utafiti wangu mdogo
nimegundua wanashindwa kuendelea kwa kuwa ya kuwa na maadui,kuna mwanamziki wa Uganda
Jose chameleon alisema ameamua kumaliza beef yake na Bebe cool kwa kuwa ina msababishia
kukosa deal kubwa za kuimba nje ya nchi na pia ndani ya nchi,hii ilikuwa yu sababu ya kuacha beef na
siyo sababu nyingine.Ndugu yangu dunia ilivyo kutokea kipindi kilichopita ni katika mtizamo wa huyu
kashinda na huyu kashindwa(win loose) na kweli mtizamo huu sio mzuri na ndoo unasababisha vita na
mtafaruku katika jamii na ndoo huu unasababisha vita tokea enzi na enzi hapa duniani lakini mimi na
wezangu baadhi ya waandishi tunasema hapana sasa ni yatosha tuanze kuishi win win sides(pande zote
zote zimesinda)hakuna aliyeshinda,nilibahatika kuangalia mashindano fulani ya mziki baadaya
kutangazwa mshindi ndipo ugomvi kupitia wasanii ukafumuka nikagundua win loose imewaathiri,hata
sasa sera ya dunia ndoo inavyosema hivyo juzi tulikuwa na uchaguzi hapa Tanzania,upande wa
zanzibar baada ya DR Shein kutangazwa mshindi Mpinzani wake Maalim Seif alisema sote
tumeshinda,wewe leo unangania uitwe mshindi yule aitwe kashindwa baada ya hapo kweli utakuwa
na amani kichwani ukifikiria adui wako?Ndugu yangu kila mwandamu anhitaji kuungwa mkono na
kupewa matumaini na mtu mwingine,chukulia wewe ni mfanya biashara unahitaji wateja wa bidhaa
zako huwezi kupata kipato kama huna wateja,je embu jiulize kama una adui wengi huoni kama ni
kizingiti katika kuogeze kipato kwako?tena inakuwa mbaya ukianzisha vita halafu huna jeshi hapa
ndugu yangu ni mbaya sana watu kumaliza kwa kubomoa misingi ya kazi yako na kufika
tamati(mwisho)pasipo kujijua na kuanza kutapatapa,Martin Luther king anasema kama huwezi
kupigana na sisi basi jiunge na sisi.Sasa ni jinsi gani ya kuungwa mkono na wengine haitaji kutumia
nguvu ili watu wakukubali njia rahisi na yenye tija ni kuwajali,kuwaheshimu na kuwathamini watu
haijalishi ni nani,kitaalamu haijalishi ni wapi anatokea Afrika,ulaya au wapi binadamu yeyote anahitaji
kupendwa na anahitaji kuona yeye wa thamani.
Zifuatazo ni njia unazoweza kutumia kuonyesha una wathamin binadamu wengine:
1.Penda kuwasalimia watu kwa vifupi vya hadhi ya majina yao mfano Mr,Mrs,Miss,Dr,Prof,Sir na
kadhalika ,wasalimu kinyenye kevu na kibusara
2.Mara zote tumezungukwa na dunia iliyo na watu wasio wakamilifu mfano kuna maneno ya
umbea,wivu,uongo sehemu tunamofanya kazi,ishi na kadhalika ndugu yangu kama huwezi kuonge
chochote kizuri au jambo jema kuhusu mtu fulani bora unyamaze kimya.
3.Usujaribu kuwapinga wengine pasipo kuwapa jibu mbadala au njia mbadala iliyo bora ,wapinge
watu katika kuwajenga
4.Mabadiliko yanaanzia kwako na kusambaa kwa wengine, anza sasa kufanya mazoezi ya
kuwathamini wengine anzia kwa mkeo,watoto wako,familia yako,marafiki wako,jirani zako,jamii kwa
ujumla....
5.Wafanye wengine wahisi kuwa wa muhimu sana na hii inakuja kwa kuwaambia kuwa una
wapenda ,unawajali na wao ni watu muhimu sana katika maisha yako nk
Ndugu yangu sisi hapa duniani tupo tofauti wenye mitizamo tofauti na inawezekana sawa ,na wakati
mwingine tupo kwa kazi zinzofanana hata kama ni hivi usichulie ni adui wako bali ni mwezako katika
kukamilisha maono yako.

DEOGRATIUS ANAWAKARIBISHA WOTE KWA SCIENTIFIC MONEY