Dashboard Builder for Access 2.0 Antivirus Report

Wednesday, February 2, 2011

Kuna jambo Linahitajika Lifanyike sasa.........



    
VITU VINAVYOFANYA ADUI UJINGA KUWATAWALA WATANZANIA WENGI
1.Kazi za magazeti ya udaku na mengine yasiyokuwa makini,Haya ni chanzo kikubwa kwa asilimia 80% ya watanzania wanayoyatmuia  hivyo kuishia kupanda mbegu ya ujinga na hivyo kupelekea kila wiki kuvuna  wajinga  wengi sana ,pia haya magazeti mengine ambayo yana andika wazo/hisia  za mwandishi kuwa  ndio tukio  na hali halisi(facts) nakuwa ndio ndoo kichwa cha habari siku hiyo na kuishia kuvuna  watu wanajiendesha kutokana na wazo la mtu(mwandishi) badala lake mwenyewe.hathari yake ya kazi  ya haya magazeti ni  kuwa na   watu wasikuwa wakuweza kuchangia mada au ajenda kwa kuwa wana taarifaa za watu sio walizojaza kichwani na sio mada/ajenda hivyo ukiwaleta katika mada ni weupe.
2.Exposure(kutoka nje ya nchi),nchi yetu ni ya uchumi huru lakini watu kiukweli bado tupo tuna fanya  na kuishi maisha ya uchumi usio huru(closed economy) watanzania karibia wote waliotoka nje ndio ambao wanaojua mambo na ndoo inasemekana ndoo wenye ushindani katika soko la dunia lakiniasilimi yao ni ndogo sana ,kama ndoo hivi tunahitaji tujiulize je kama tunataka kuendelea wakati wanafunzi wanaofanya exchangeprogramnje ya nchi ni wachache,wanaoenda kusoma ni wachache,kufanya kazi bado ni wachache je tutawezaje kuendele kutoka hapa tulipo?muda sasa umefika kuanza kupeleka ndugu zetu nje ya nchi kwa wingi wakaitangaze  na kuleta teknolojia mpya na mawazo tofauti nakusababisha kuwa na taifa la wajanja,inasemekana nchini Nigeria karibia kila mnaigeria ni mjanja hakuna wa kumdanganya.
3.Kutokuwa na muda wakufikiri angalau nusu saa kwa siku,Tanzania maeneo ya wazi kwa umma ya kumpuzika  ni madogo na machache sana mjini jua kali wiki nzima watu wapo resi n a maisha yao  litakalo tokea kesho au baadae na liwe,watu wengi ni waathirika wa brain drain,muda  wa kufikiri hakuna na kama kam hujafikiril eo kesho kuna mtu atakufikiria na kukutawala .Sasa nini tufanye kwa hili tutenge maeneo mengi ya wazi kwa mapauziko kwa watanzania,elimu kupitia media juu ya umuhimu wa kufikiri tukumbuke kama hatufirii leo kesho mtu atafikiria na kukutawala.
       
4.Kusoma vitabu,kuna msemo wa siku nyingi unasema kama unataka kumficha mwafrika basi weka ujumbe kwenye kitabu,mara zote kama uantaka ukombozi wa kimaarifa basi huna budi kujifunza kutoka kwa wengine na wewe pia ujue nini ufanye ili ulete mabadiliko tofauti,kuna aina tofauti za vitabu kwa watu wa dini vitabu vyao vitakatifu bado  hata theluthi hawafikia walio wengi,muda sasa umefika acha kupenda kusikiliza anzan sasa kusoma mwenye ili uwe huru,nunua vitabu kuna vya kukusaidia wewe ufanikiwe kifedha,furaha,siasa,historia za mashujaa mbalimbali,mara ya kwanza utaona kawaida lakini kadri unavyozidi kuendelea kusoma vitabu ndoo yanakuwa maisha yako  ya kila siku na kuwa sawa na kuamka mara ya pili.
5.Mfumo wa elimu na sera ,mfumo wetu  unahitaji mabadiliko sana katika hii dunia ya utandawazi,ndio kuna dunia ziliendelea kwa lugha zao lakini mimi sina maana tukitupe Kiswahili bali ni kama tuna cheza mchezo wa makusudi wa kutengeneza matabaka  katika jamii,mfumo unahitaji kubadilika  mfano masomo yote yanatakiwa kufundishwa kwa kiingiingereza kuanzia chekechea,primary na kuendelea, huwezi kumfundisha mtu kiingereza na wote wakajua kiingereza wakati umri wa wao (kipindi mototo ubongo wake una elewa zaidi sana umepita yaani kakomaa tayari)ni sawa na mafunzo ya sarakasi kama hukufanya ukiwa mdogo viungo bado havijakomaa  ukija ukubwani kama ukifanikiwa itakuwa kwa shida sana na dunia kuanzia china ,japan ,urusi,kote huku sasa watu wanaongea kiingereza,tuanze sasa kujifunza English  maaana mambo mengi yameandikwa kwa kiingereza.Wazazi tafuteni shule za English medium wakasome maana taifa la kesho kama hamjafanya hivyo watoto wenu watatupwa nje ya mfumo msifurahie shule za kata ni mtego wa kutengeneza tabaka la tatu kubwa


    
6.Meditation,meditation ni muhimu sana kwa taifa kama hili,kwa maendele yaliyo bora na kuwa huru meditation inahitajika,mara nyingi tunapata stress tutokapo makazini,miangaikoni,tuna hitaji meditation ili kuondokana na haya yote,pia kuirefresh akili zetu zianze upya.kuwa na fikra sahihi
7.Kazi inayofanywa  na television na redio station,maisha ya siku hizi taarifa ndio ufunguo wa maisha na sio tena elimu ya darasani(formal education) japo kuwa inaumuhimu pia,television  na redio station zinafanya kazi ya  kusambaza hizi taarifa kwa asilimia kubwa ya watanzania,lakini sio taarifa za kufanya wao wawe bora na wajanja sana katika hiii dunia,kuna siku nilibahatika kutizama  kituo kimoja cha television mtangazaji aliyekuwepo pale yaani wewe ndoo unatakiwa umuambie au ndoo umpe data  ilikuwa inatia huzuni kwa mtu kupewa mamlaka ya kutangaza halafu hakuna kitu kichwani alichofanya juhudi aweke ili awaaambie watu,tunahitaji kufanya mabadiliko katika vyombo vetu vya habari kuzifanya taarifa za kuwaza kijanja na kisasa na kujenga mtu.
BOB MARLEY ni mmoja kati ya watu waliofanya mapinduzi ya fikra sana kwa watu weusi na hivyo kupelekea  watu wengi kuwa  ya kuheshimiana kuna msemo mmoja wake anasema “every men got right to decide his own density”je wewe unataka nini  na vipi kusuhusu density yako?jikomboe sasa usije ukaibeba dunia.....,jiulize sasa wewe unaionaje dunia sasa?chukua hatua

 KANUNI   INAYOTUMIWA  NA WANASIASA  WENGI  KUWAMALIZA   MAADUI  ZAO:

Mihemuko ya kisiasa kama wewe ni mwanasiasa na haupo imara na jasiri(makini) inaweza kukupelekea kuchafuka na kutokuwa na thamani kwa wateja  ambao ni wananchi wapiga kura wan chi yako au jimbo na kata yako,siasa ni biashara kama zilivyo biashara nyingine mfano kuna muuza sera na wanunua sera kwa hiyo mwanasiasa ni mfanyabiashara wa kuuza sera wananchi  ni wateja,nimekuwa karibu kufuatilia siasa za Afrika,east Europe,Asia,Uarabuni,na nchi za magharibi ambapo ndipo wanafilisophia wa demokrasia wengi wametokea huko,na katikamaeneo haya yote siasa zinatofautia hii inatokana na sababu nyingi sana za msingi baadhi ni umriwa demokrasia katika bara na nchi husika,utamaduni, na uhuru wa maamuzi kwa wananchi na vingozi wanchi,mara kadhaa nimeshudia wateja wa wanasiasa wakiwashusha thamani wanasiasa na kuwapandisha lakini siri nzito huwa inabaki ndani wale wanaopanga mara  nyingi katika kila maamuzi asilima themanini huwa ndio waanga wa jambo lolote lile,kuna sehemu kama nchi za SADC  wapinzani mara zote hutumia principle za kisaikologia za kisiasa katika kutimiza haja zao japo bado idadi sii kubwa sana ya wanasisiasa wanaojua nini maana ya demokrasia na uchaguzi,katika kanuni zote nii hii ambayo mimi huiita” pima”yaani  ya kumtupia adui mtu(mpizani wako)neon la kashfa Fulani au neon la mtego na kama mpizani wako si makini ataingia kichwa kichwa kukujibu na na kujikanyaga kanyaga kukupatia nguvu ya wewe kuweza kusonga mbele   na kukuacha wewe umeshuka thamani k awateja wako  hapa sina maana kuwa unatakiwa kuwa kimya muda wote  bali upo katika mazungumzo gani?mwaka 2010 novemba  Obama  raisi wa marekani  nchi yake siri za ubalozi zake zilivujishwa lakini yeye kama yeye alikaa kimya kutojibu chochote maana yake jibu au maoni yake na msimamo wa serikali yake ungelete mzozo dunia nzima maana hapa kuna watu wampinga Lusian Assange na watu  wengine  wanataka uhuru  wa vyombo vya habari na wote wana  hoja  za msingi kulingana  na wote hawa,hivyo kama thamani yake ingeweza kuporomoka kwa kasi kubwa sana,Kitaalamu mtu akikutupi neon baya na wewe ukiruhusu kupita jambo hilo kupita ndani ya sehemu za ufahamu kao na nafsini kwako huwa ndoo kamba ya kujinyonga nao umejitundika nayo, hapa kweli mara nyingi watu hufanya makosa kwa kuchanganya kupita kiasi malengo yao dhidi ya matatizo ,sasa ndugu yangu napenda kukuambia kuwa  angalia ni mada ipi unaenda kuzungumza na watu zaidi ya wawili au jamii na wewe unanafasi gani katika hilo usije ukajifanya wewe ni redio mbao ukaishia  huna thamani,Nchini Tanzania katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 october  mkurugezi wa jeshi la wananchi wa Tanzania aliwahi kuogea kwa mihemko  ya kijeshi  kuonyesha kama anakilalia chama Fulani mfano CHADEMA  ,alichofanya DR Slaa ni kutumia nafasi hiyo kumtupia neon lisilo la kumuhukumu bali ni kumtega ili aende katika vyombo vyombo ya habari ili ajibu na kujikanyaga Dr Slaa alimuuliza aseme  fedha za meremeta na nyingine aleze ziko wapi?kwa saikolojia ya wengi walikuwa wanategemea mkurugezi wa jeshi angejibu bali  hakujibu,lakini kila pale Dr  Slaa alipoendele kumchokonoa  ili mkurugenzi lakini mkurugezi aliendelea kukuaa kimya  maana mkurugezi wa jeshi  alikuwa anajua kama angejibu basi ingekuwa ni kitanzi chake  kwani lilokuwalinafuata ni yeye kupoteza thamani,umarufu kwamaana hata kama vipi yeye yupo sahihi watu hawataweza kumuelewa yeye.Mara nyingi kuna watu maarufu Tanzania wamekuwa na kashfa nyingi   kupitia magazeti na mwishoe kupoteza wateje wao na  umaarufu wao nchi nzima na watu kuwaona kichefuchefu  hii ni kutokana na wao kidogo tu wakiandikwa vibaya wanakimbilia katika vyombo hivyo hivyo kujibu wakifiri wametatua tatizo kumbe wameliongezea hatua tatizo,ndugu yangu najua elimu juu utumizi wa vyombo vyombo  vya habari Tanzania bado ni ndogo,tumia sasa vyombo hivi kukujemnga wewe na sio kukubomoa penda hisia zako mfano umechukia usionyeshe tawala hisia zako,kuwa mtu kuongea chanya muda wote,kama huna neon lolote nzuri kwa Fulani au kwako usiogee kabisa siku hiyo,kuwa huru na maneno ya watu wewe ni tofauti na wengine.Mtu aliyekuwa huru ni mtu anayefanya maamuzi yake kwa kutakari tamani sasa kuwa makini kwa lolote lile ambalo unakutana nalo katika  sekta ya siasa
.

Ni vizuri....

kwa kuiga”hakuna jambo
 

TUEPUKE KUISHI KWAMAJIBU TUISHI KWA MALENGO YETU:
Katika jamii tunamoishi kuna mambo mengi mazuri na mabaya hakuna jamii iliyo kamili pasipo doa,lakini
jambo la msingi najiuliza swali katika jamii yangu ya kiafrika kwa nini hatuendelei?katika tafakari ya
ngu na tafiti zangu kwa kujinasibu kabisa niligundua sisi Afrika tunapenda kuishi kimajbu kuliko
kisulu na kusababisha kuchelewa kwa uvumbuzi na kuwa na mambo machache sana yale yale
yaliyozoeleka na ya kawaida sna kwa jamii za wenzetu,mathalani katika kila sekta na sehemu wengi
mtu akianzisha jambo wengine wanaiga au kujibu kutengeneza jambosawa na lile,ofisi fulani
ikianzisha system fulani ya mfano kutunza vitabu vya uhasibu zingine zinajibu kwa kuanzisha
programu sawa wakati programu zipo kibao sana,au katika mtaa ukinunua nguo fulani sana sana kwa
akina mama jirani yake haraka haraka kesho anaenda dukani na kununua na kadhalika,haya ndugu
yangu si maisha ambayo tumeitiwa ,maana kila mtu duniani yupo tofauti na mwingine hapa
duniani,huwezi kuniambia kikwete akaweza kufanya sawa kama nyerere kamwe haiweekani,kila
mwanadamu yupo unique kutoka kwa mwingine ndoo maana unakuta wanafunzi darasani mwanafunzi
alikuwa wa mwisho lakini katika michezo anashika nambo moja.Nndugu yangu acha kuiga au kulipa
kisasi fuata malengo yako yanavyosema kwani ukiiga unakuwa na photocopy tu original ya jambo hilo
lile huwa anakuwa analoyule mwanzishaji wa jambo,kuna mwanazuoni mmoja anasema kama kama
hujui mwekekeo unaoelekea njia yeyote inaweza kukuchua kwa kuwa huna malengo ya unapoelekea.
Ndugu yangu kuwa na msimamo wako,tafuata sasa kuwa na mtazamo chanya hasa pale watu
wanafikiri haiwezekani wewe tafuta kuweza na kisha utaona jinsi utakavyofanikiwa kimaajabu,ndugu
yangu maneno huumba unavyofikiria ndivyo itakavyo kuwa tafuta sasa suluhu,watu wengi hawapendi
kwenda ile njia ngumu wanapenda raisi ndoo maana wanaishi kimajibu”
zuri lenye mafanikio duniani linakuja kirahisi raisi,acha sasa fikra ya kusema nataka kuwa kama
mfanya biashara fulani hujui alipoanzia na kupata fedha zake,taka kuwa kama wewe kwa kuwa hakuna
kama wewe duniani na hakuna uliyefanana naye duniani ila kuna mambo ya kujifunza kutoka kwa
wengine hapo jifunze lakini sio kuiga tena kiharamia,fursa zipo nyingi sana hapa afrika kuliko sehemu
nyingine duniani anza sasa kuzichangamkia ,kuna mwanafuzi mmoja wa nairobi university alikuwa
ananiambia Deo nikiitizama Afrika naitamani kwa kuwa nisehemu rahisi ya kutengeneneza fedha ,acha
fikra za kwenda ulaya ukifiri utakuwa tajiri ,jiulize matajiri wa kuwe wana mifumo tayari ya kufyonza
fedha katika vyanzo kedekede je utaweza pambana nao kama wewe huna mfumo wa kufyonza fedha?
acha lalamika eti huna mtaji haichukui fedha kutengeneza fedhe bali inachua wazo kutengeneza
fedha,anza kidogo na wazo lako la kibiashara na kisha lifanyie kazi utaona kama hutofanikiwa ndugu
yangu wazo ni fedha changamkia sasa itakuwa nikweli kwako msemo wa Disraeli kuwa Life is too
shot to be small,na kuelekea kwenya mafanikio mar nyingi unakutana na upinzani mkali unaweza
kuwa wa kiroho,familia,na unaweza kuwa wa wazi wazi au ulijificha lakini upo,usipo kuwa makini
unaweza kutafuta majibu pasipo kutafuta suluhu,wengi matajiri wa sasa hapa mjini mfano kariakoo na
posta walikuwa na idea ya kujenga maghofa lakini mtaji walikuwa nao mdogo,lakini walijua punde tu
watakapo jenga msingi wateja watajitokeza kuja kuweka order nahatimaye wale wateja waliokuwa
wanaweka order ndio waliokuwa wana toa fedha ilikuwa inamalizia jengo nzima hii ndio siri kubwa
duniani ndugu yangu,ideas ndizo zinatengeneza fedha na sio fedha kutengeneza fedha,amka usingizini
karibu katika dunia ya mafanikio karibu karibu ,tiketini wazo lako la kibiashara hiyo ndio dira yako
iweke kwa maandishi maana ni ramani ya njia utakayo pita isije njia nyinge ikaja ikakuzoa zoa.