Dashboard Builder for Access 2.0 Antivirus Report

Thursday, December 23, 2010



                                        MAFANIKIO HAYAJI PALE ULIPO UNAFUATA:
Mwenda  buresi kama mkaa bure,huwa anaogeza maarifa na kujifuza zaidi mithali ya Kiswahili inamaana kubwa sana ,ni ndoto au wishes za kila mtu kuwa na mafanikio makubwa sana duniani,lakini kuna tofauti na watu wenye  malengo yaliondikwa kwa karatasi na kuanza kuyatekeleza hawa hugeuza wachotaka kuwa  kuwa kweli  nakuruhusu  mabadiliko ya mafanikio  katika maisha yao,dunia ilivyo sasa ni utandawazi ,taarifa ndio ufunguo wa maisha na sio elimu tena kama ilivyokuwa awali kama huna taarifa juu jambo Fulani basi sahau kuhusu hilo jambo kulifanikisha,mathalani  nilikuwa Kenya nilikutana na Wagerman wengi sana lakini kilichonifurahisha wengi wao walikuwa ni wanafunzi wa political science,sababu tu pekee walioniambia kwa nini walienda Kenya ilikuwa  ni kutaka kuwa bora katika soko laajira linalowangoje baadaye,katika hali za kawaida  mara nyingi huwa tunasikia matangazo ya ajira za kimatifa lakini ni wangapi ndugu zetu huwa wanafikia viwango vyakuchaguliwa  achana na vile vya kisiasa ambavyo huwa tu mtu huchagua kwa kuwa alijifunga na ahadi zake tuje hizi unaenda kushindana na wenzako mnapewa nafasi sawa wengi huishia sakafuni sababu tu  ya kile wanachokijua bado ni kidogo,ndugu zetu huwa  mara nyingi wanaoshiriki  mashindano ya kimataifa  mfano zain Africa challenge huwa hurudi ni kwa sababu tu wamekosa nini jiulize?mara nyingi ndugu zetu huishia kusoma na kukariri sana na kusahau kuwa mbona wapinzani wao hawatumii njia wanayotumia  huwa watu wan chi zinazochukuwa huwa  wanafunzi wao  huwa yale maswali wanayoulizwa huwa ni maisha yao  ya kila siku na sio kama kuanza kuingia mitandaoni kusoma na kwa kukesha .
   Ndugu yangu kwa mantiki hii dunia  imekuwa utandawazi,watu sasa wanapigania kuijua mitaa ya hiki kijiji ili wajue ni jinsi gani wataweza kusurvive katika hiki kijiji,kama wewe unafahamu tu mkoani kwao tu,je jiulize leo utaweza kushindana kibiashara,soko la ajira na mtu aliyetembea nchi zaid kumi?utapotea na kumezwa tu kwa maana huyu  aliyetembea ,mitaa mingi zaidi anaijua njia vema,kwa namna yeyote ile ufuhamu utatofautiana,huyu atakuwa na kadunia kake na Yule atakuwa na dunia yake ,ni muda sasa wa kuchukua hatua ndugu yangu ,utafiti unaonyesha watu  ambao wameishi katika makazi yao toka wazaliwe na kuishi hapo hapo mpaka uzeeni kwao uwelewa wao wa mambo  unakuwa mdogo na wakubabaisha,na pia mimi nasema kuwa mafanikio yao ni madogo  huishia katka janga la umasikini wa kujitakia maana ndio umasikini afrika upo,katika uchunguzi wangu niliufanya katika kulinganisha watu wa aina mbili mmoja kaishi ulaya na mwingine kaishi Tanzania  umri wao wote niligundua tofauti ya uelewa ipo kubwa kati ya pande mbili,hivyo katika  watu wanaoishi kijiji kimmoja maisha yao yote hapa Tanzania   na wale waliohama kijiji mara kwa mara ulewa wao na mafanikio yao huwa ni tofauti ndugu yangu tupo katika dunia mambayo ni lazima  ili ufanikiweuweze kujua wezako wako wapi ili uweze wewe kupiga hatua,hii  ndoo jibu tosha la wewe kuweza kufunguka maishani mwako exposure ni muhimu,katika nchi yetu inasemekana kuwa asilimi kubwa  ya waliopata exposure nje ya nchi ndoo waiendesha  nchi hii    ndugu yangu napenda kukuambia kuwa kuwa mafanikio hayaji tu pale ulipo bali wewe unayafuata yalipo,acha kuku mtaani muda wote,acha kukuaa nyumbani masaa yote toka nje uyafuate mafanikio jichangane katika social event,music concerts,national events na kadhalika utapata kufunguka hakika,acha leo kuwa na maisha ya pembe tatu,yaani kuwa na ratiba fixed,mfano ukitoka kazini au shuleni unaelekea nyumbani na sehemu ya mwisho kuhudhuria ni maeneo ya dini,haya sio maisha ni kama upo kwenye gerza lako wewe mwenyewe,jifungue sasa upate kufunguka na kufanikiwa,mathalani kama wewe ni majsiriamali anza sas kuhuudhuria international event/exhibition,penda kujuana na wengi pasipo kikomo,kuwa tayari ya kulipia gharama ya mafanikio yako an uweze kupata funguo ya mafanikio yako.

Memory zetu inawezekana kuwa fanisi


                         JINSI YA KUWA NA KUMBUKUMBU VIZURI :
Mwaka  2009 nilikuwa mzumbe university nilikuwa katika somo la IT(Information technology)nikapata wazo kama kweli vichwa vetu vingekuwa ni komputa kirahisi tu ningewashauri watu waongeze chip za komputa  ili kuongeza kiwango cha kutunza kumbukumbu vichwani(ubongoni) mwao,lakini ubongo wa mwanadamu ni mashine ambayo  ipo na mambo chungu nzima kuliko kifaa/mashine yeyote ile ya kisasa,hivyo basi kama mtu anataka kuboresha kumbukumbu kichwani anahitaji juhudi Fulani hivi,chukulia mfano ni kama mtu anayekwenda  kufanya mazoezi ya kunyanyua  vitu vizito kadri anavyo zidisha  na kuweka juhudi ndoo  mishipa na misuli yake inavyozidi kutanuka hivyo hivyo katika kuboresha utunzaji wa kumbukumbu inafanya kazi wa kukumbuka unaongezeka kadri unavyofanya mazoezi ya kutunza vizuri kumbukumbu.Kuna aina kadhaa ya vitu vya kutunzia kumbukumbu mfano twasira ya picha,sentensi,mizaha,njia za loc, nk.Zifuatazo ni  namna  mbalimbali za kuboresha utunzaji wa kumbukumbu vizuri:
 1.Mazoezi ya mara kwa mara,husaidia kuongeza oxygen kwenye ubongo ,hivyo kupunguza majanga ambayo  hupeleke kutoke kupoteza kumbukumbu mfano wa magonjwa  kama kisukari na  cardiovascular.
2.Jaribu kuthibiti msongo wa mawazo(stress),Msongo hupelekea kuharibu hippocampus zetu,pia msongo wa  mawazo hupelekea kuwa ni vigumu mtu kulifuatilia jambokwa umakini,hapa nashauri kufanya meditation inasaidia kutatua tatizo.
3.Kuwa na tabia ya kulala vema,kulala ni muhimu sana katika kuimarisha utunzaji mzuri wa kumbukumbu ,ulalaji wa chini ya masaa saba unasababisha mtu kushindwa kufuatilia jambo kwa umakini pia ulalaji wa kupitiliza masaa nane  mfano mtu kulala masaa tisa husababisha matatizo.
4.Acha tabia ya kuvuta sigara,uvutaji wa sigara huzidisha matatizo katika viungo vyetu  ambapo hupelekea mtu kupata magojwa ya mshituko(stroke) na pia kuziba mishipa inayokwenda kupeleka oxygen kwenye ubongo.
5.Kula vizuri na sahihi,tafiti  zinaonyesha kuwa kuna aina za vyakula vinavyo saidia kuboresha utunzaji wa kumbukumbu ,mfano matunda,mboga za majani,wanga, nk,vitamin B san asana B6 na B12 mfano spinachi,melon,maharagwe ya soya,matunda ya citrus nk,pia vitamin C and E mfano nyanya za nyekundu,karanga,mbegu,samaki wa maji baridi,na mafuta ya walnut
6.Husiasha viungo vingi ikiwezekana,hata kama wewe unajifunza kwa kutizama  soma unachojifunza kwa sauti  kile unachotaka kukumbuka,hata kama unaweza kukiwekea katika melodi ya nyimbo ili ukiimbe fanya hivyo,hapo  utakuwa umehusisha viungo kama macho,mdomo,mkono nah ii inasaidia sana  mambo yakiwa mengi hujui la kufanya nk.
7.Pangilia taarifa zako,jaribu kuandika taarifa zako kwenye kitabu kwa mpangilio wa tarehe na  taarifa nyingine muhimu.
8.Penda kuwa muelewa  ,achana na tabia ya kukariri anza na  kuweka tabia ya kuelewa jambo na kuliweza kulieleze kwa lugha yako  mwenyewe.
9.Husisha kile ulichokielewa na  kwa kiunganisha na taarifa mpya kwa taarifa ulielewa kabla ili kutengeneza kitu kimoja kikamilifu.
Kulingana na tafiti mbalimbali  wanadamu wengi inasemekana hutumia asilimia ndogo sana  ya ubongo wao hii utokana na uvivu,au kukosekanika kwa maarifia,mfano  katika asilimi mia  mwanadamu wa makamo hutumia asilimia tano tu,hii nyingine hubaki bila kutumika ,anza sasa kuutumia ubongo wako ukuuletee mabadiliko,wewe unauwezo mkubwa sana wa kutunza kumbukumbu na kuweza kuletamabadiliko anza leo.

Monday, December 20, 2010

hakika furaha ya kweli ni haki yako , an ya kila mtu....



JINSI YA KUPATA FURAHA YA KWELI
Mama Teresa anasema peace begin with smile!na je wewe ushawahi kujiuliza siri ya furaha ya
kweli ni nini?Kuna siku ulishawahi kujiuliza furaha siri yakeni kuwa na fedha tu?vipi kuhusu
umaarufu,nafasi katika madaraka ya nchi au kampuni fulani maarufu hapa Tanzania,je hivi vyote na
vingine vingi vyaweza kukupa furaha ya kweli?Lakini mbona ndoa za matajiri kama Donald Trump na
watu maarufu duniani hazidumu au hazina furaha?achana na hilo mbona pia ndoa na familia za watu
masikini wengi pia zimekosa furaha? Hapo hapo kuna matajiri kama Bill Gates na pia watu wenye
kipato kidogo sana kama Mama Teresa wana furaha sana duniani,ndugu yangu dunia imetengenezwa
kwa kanuni na pi mambo ya dunia yote yana kanuni ukiwa nje ya kanuni hizo katu huwezi kunufaika
nazo,siri ya furaha ya kweli ni maarifa ambayo mtu unatakiwa ujifunze na sio mtu anazaliwa
nayo,maarifa yafuatayo ukiyafuata nina uhakika utapata furaha ya kweli:
Penda kujitolea katika kazi za kijamii,kuwa mstari wa mbele katika mambo ya
kijamii,muungwana,kusaidia wana jamii mfano unaweza kwenda hospitalini ukaenda kuwajulia ali
wagonjwa na kuwapa msaada.
Jipende kwanza wewe,usiwe mgumu juu yako,hakuna mtu mkamilifu,Grace Matata anasema
kujipenda inaanzia kwa mimi kisha upendo unasambaa kwa wengine,penda maisha katika hali zake
zote,
Usiupe nafasi ushauri hasi uingie nafsini kwako,tumezungukwa na dunia isiyo na watu
wakamilifu,kuwa mtu muwelewa wakati mwingine tunaofautiana kwa sababu ya mtizamo
tofauti,ukitaka kujiweka katika nafsi ya mtu kutaka kujua kwa nini manasema hivi au vile unaelekea
kuvunja ukuta wako wa chuki,yasikusumbue maoni mabaya ya mtu kamwe.
Penda kuwa rafiki wa kila mtu,kuwa rafiki kwa kila mtu unayekutana naye,kuwa rafiki
haimaanishi kuwa kila unayekutanaye umpeleke kwenu la hasha bali kuonyesha tabia njema mbele ya
wengine,mwandishi mmoja anasema,when you give positive vibes you will attract positive vibes.
.Kuwa wewe mwenyewe,usipende kujilinganisha na wengine,kila mtu yupo tofauti hapa duniani
hakuna aliyefanana na wewe au uliyefanana naye,jisikie vizuri na njema kuwa wewe unakila kitu
ukijumuishana roho nzuri.
Samehe na sahau,mathalani upo ndani ya daladala mtu kakukanya mguu na kukuomba
msamaha samehe,kusamehe sio kazi rahisilakini ukisamehe unapata ghafla amani ya moyo,samehe
kwa manufaa yako kama siyo ya wale.
Fikiri chanya muda wote,prof wangu chuoni Mzumbe, prof mevdshet anasema positive is more
powerful than negative, mara zote ukiongea hasi unonyesha kwa watu nini kimepungua ndani
yako,nguvu ya chanya itakufanya kila ufanyalo ufanikiwe pasipo kipingamizi kitakacho athiri furaha
yako.
Acha kuweka assumption,kumfikiria mwezako vibayo au kumwekea makadirio mabaya
itakuletea maumivu juu yako mambo yatakopakuwa tofauti na unavyohisi,dunia hii ya watu wastaarabu
na wewe ni mmoja wapo watu huwa wanaongea kwa mamlaka fulani yaani kwa ushahidi na sio
minongono na lawama zisizo za kweli.
Usichukilie vitu kibinafsi,mimi huwa nasema ukisha kuwa maarufu yaani unafahamika kwa
zaidi ya watu wawili,hapo tena una share maisha na wengine hivyo angalia unapofanya maamuzi si
kama wewe bali kundi zima unalo-share nalo maisha linufaike na maamuzi hayo
Ndugu yangu asilimia kubwa ya watu duniani masikini na matajiri huwa mara nyingi wanajikuta
wanaishi maisha yasiyo na furaha na kutamani kujiua mara nyingine sababu huwa ni ndogo sana
kukosa maarifa kuwa kutokuwa na furaha ni wao wenyewe walichagua,pia vilevile unapoona mtu an
furaha ujue pia amechagua hayo maisha,chagua sasa furaha ya kweli,kwani mtu mwenye furaha ya
kweli ni mtu mwenye mafanikio makubwa sana hapa duniani.
                                              Tyra moja ya show zake