Dashboard Builder for Access 2.0 Antivirus Report

Monday, December 20, 2010

hakika furaha ya kweli ni haki yako , an ya kila mtu....



JINSI YA KUPATA FURAHA YA KWELI
Mama Teresa anasema peace begin with smile!na je wewe ushawahi kujiuliza siri ya furaha ya
kweli ni nini?Kuna siku ulishawahi kujiuliza furaha siri yakeni kuwa na fedha tu?vipi kuhusu
umaarufu,nafasi katika madaraka ya nchi au kampuni fulani maarufu hapa Tanzania,je hivi vyote na
vingine vingi vyaweza kukupa furaha ya kweli?Lakini mbona ndoa za matajiri kama Donald Trump na
watu maarufu duniani hazidumu au hazina furaha?achana na hilo mbona pia ndoa na familia za watu
masikini wengi pia zimekosa furaha? Hapo hapo kuna matajiri kama Bill Gates na pia watu wenye
kipato kidogo sana kama Mama Teresa wana furaha sana duniani,ndugu yangu dunia imetengenezwa
kwa kanuni na pi mambo ya dunia yote yana kanuni ukiwa nje ya kanuni hizo katu huwezi kunufaika
nazo,siri ya furaha ya kweli ni maarifa ambayo mtu unatakiwa ujifunze na sio mtu anazaliwa
nayo,maarifa yafuatayo ukiyafuata nina uhakika utapata furaha ya kweli:
Penda kujitolea katika kazi za kijamii,kuwa mstari wa mbele katika mambo ya
kijamii,muungwana,kusaidia wana jamii mfano unaweza kwenda hospitalini ukaenda kuwajulia ali
wagonjwa na kuwapa msaada.
Jipende kwanza wewe,usiwe mgumu juu yako,hakuna mtu mkamilifu,Grace Matata anasema
kujipenda inaanzia kwa mimi kisha upendo unasambaa kwa wengine,penda maisha katika hali zake
zote,
Usiupe nafasi ushauri hasi uingie nafsini kwako,tumezungukwa na dunia isiyo na watu
wakamilifu,kuwa mtu muwelewa wakati mwingine tunaofautiana kwa sababu ya mtizamo
tofauti,ukitaka kujiweka katika nafsi ya mtu kutaka kujua kwa nini manasema hivi au vile unaelekea
kuvunja ukuta wako wa chuki,yasikusumbue maoni mabaya ya mtu kamwe.
Penda kuwa rafiki wa kila mtu,kuwa rafiki kwa kila mtu unayekutana naye,kuwa rafiki
haimaanishi kuwa kila unayekutanaye umpeleke kwenu la hasha bali kuonyesha tabia njema mbele ya
wengine,mwandishi mmoja anasema,when you give positive vibes you will attract positive vibes.
.Kuwa wewe mwenyewe,usipende kujilinganisha na wengine,kila mtu yupo tofauti hapa duniani
hakuna aliyefanana na wewe au uliyefanana naye,jisikie vizuri na njema kuwa wewe unakila kitu
ukijumuishana roho nzuri.
Samehe na sahau,mathalani upo ndani ya daladala mtu kakukanya mguu na kukuomba
msamaha samehe,kusamehe sio kazi rahisilakini ukisamehe unapata ghafla amani ya moyo,samehe
kwa manufaa yako kama siyo ya wale.
Fikiri chanya muda wote,prof wangu chuoni Mzumbe, prof mevdshet anasema positive is more
powerful than negative, mara zote ukiongea hasi unonyesha kwa watu nini kimepungua ndani
yako,nguvu ya chanya itakufanya kila ufanyalo ufanikiwe pasipo kipingamizi kitakacho athiri furaha
yako.
Acha kuweka assumption,kumfikiria mwezako vibayo au kumwekea makadirio mabaya
itakuletea maumivu juu yako mambo yatakopakuwa tofauti na unavyohisi,dunia hii ya watu wastaarabu
na wewe ni mmoja wapo watu huwa wanaongea kwa mamlaka fulani yaani kwa ushahidi na sio
minongono na lawama zisizo za kweli.
Usichukilie vitu kibinafsi,mimi huwa nasema ukisha kuwa maarufu yaani unafahamika kwa
zaidi ya watu wawili,hapo tena una share maisha na wengine hivyo angalia unapofanya maamuzi si
kama wewe bali kundi zima unalo-share nalo maisha linufaike na maamuzi hayo
Ndugu yangu asilimia kubwa ya watu duniani masikini na matajiri huwa mara nyingi wanajikuta
wanaishi maisha yasiyo na furaha na kutamani kujiua mara nyingine sababu huwa ni ndogo sana
kukosa maarifa kuwa kutokuwa na furaha ni wao wenyewe walichagua,pia vilevile unapoona mtu an
furaha ujue pia amechagua hayo maisha,chagua sasa furaha ya kweli,kwani mtu mwenye furaha ya
kweli ni mtu mwenye mafanikio makubwa sana hapa duniani.
                                              Tyra moja ya show zake

No comments:

Post a Comment

THIS IS YOUR PLACE TO COMMENT