Dashboard Builder for Access 2.0 Antivirus Report

Thursday, December 23, 2010

Memory zetu inawezekana kuwa fanisi


                         JINSI YA KUWA NA KUMBUKUMBU VIZURI :
Mwaka  2009 nilikuwa mzumbe university nilikuwa katika somo la IT(Information technology)nikapata wazo kama kweli vichwa vetu vingekuwa ni komputa kirahisi tu ningewashauri watu waongeze chip za komputa  ili kuongeza kiwango cha kutunza kumbukumbu vichwani(ubongoni) mwao,lakini ubongo wa mwanadamu ni mashine ambayo  ipo na mambo chungu nzima kuliko kifaa/mashine yeyote ile ya kisasa,hivyo basi kama mtu anataka kuboresha kumbukumbu kichwani anahitaji juhudi Fulani hivi,chukulia mfano ni kama mtu anayekwenda  kufanya mazoezi ya kunyanyua  vitu vizito kadri anavyo zidisha  na kuweka juhudi ndoo  mishipa na misuli yake inavyozidi kutanuka hivyo hivyo katika kuboresha utunzaji wa kumbukumbu inafanya kazi wa kukumbuka unaongezeka kadri unavyofanya mazoezi ya kutunza vizuri kumbukumbu.Kuna aina kadhaa ya vitu vya kutunzia kumbukumbu mfano twasira ya picha,sentensi,mizaha,njia za loc, nk.Zifuatazo ni  namna  mbalimbali za kuboresha utunzaji wa kumbukumbu vizuri:
 1.Mazoezi ya mara kwa mara,husaidia kuongeza oxygen kwenye ubongo ,hivyo kupunguza majanga ambayo  hupeleke kutoke kupoteza kumbukumbu mfano wa magonjwa  kama kisukari na  cardiovascular.
2.Jaribu kuthibiti msongo wa mawazo(stress),Msongo hupelekea kuharibu hippocampus zetu,pia msongo wa  mawazo hupelekea kuwa ni vigumu mtu kulifuatilia jambokwa umakini,hapa nashauri kufanya meditation inasaidia kutatua tatizo.
3.Kuwa na tabia ya kulala vema,kulala ni muhimu sana katika kuimarisha utunzaji mzuri wa kumbukumbu ,ulalaji wa chini ya masaa saba unasababisha mtu kushindwa kufuatilia jambo kwa umakini pia ulalaji wa kupitiliza masaa nane  mfano mtu kulala masaa tisa husababisha matatizo.
4.Acha tabia ya kuvuta sigara,uvutaji wa sigara huzidisha matatizo katika viungo vyetu  ambapo hupelekea mtu kupata magojwa ya mshituko(stroke) na pia kuziba mishipa inayokwenda kupeleka oxygen kwenye ubongo.
5.Kula vizuri na sahihi,tafiti  zinaonyesha kuwa kuna aina za vyakula vinavyo saidia kuboresha utunzaji wa kumbukumbu ,mfano matunda,mboga za majani,wanga, nk,vitamin B san asana B6 na B12 mfano spinachi,melon,maharagwe ya soya,matunda ya citrus nk,pia vitamin C and E mfano nyanya za nyekundu,karanga,mbegu,samaki wa maji baridi,na mafuta ya walnut
6.Husiasha viungo vingi ikiwezekana,hata kama wewe unajifunza kwa kutizama  soma unachojifunza kwa sauti  kile unachotaka kukumbuka,hata kama unaweza kukiwekea katika melodi ya nyimbo ili ukiimbe fanya hivyo,hapo  utakuwa umehusisha viungo kama macho,mdomo,mkono nah ii inasaidia sana  mambo yakiwa mengi hujui la kufanya nk.
7.Pangilia taarifa zako,jaribu kuandika taarifa zako kwenye kitabu kwa mpangilio wa tarehe na  taarifa nyingine muhimu.
8.Penda kuwa muelewa  ,achana na tabia ya kukariri anza na  kuweka tabia ya kuelewa jambo na kuliweza kulieleze kwa lugha yako  mwenyewe.
9.Husisha kile ulichokielewa na  kwa kiunganisha na taarifa mpya kwa taarifa ulielewa kabla ili kutengeneza kitu kimoja kikamilifu.
Kulingana na tafiti mbalimbali  wanadamu wengi inasemekana hutumia asilimia ndogo sana  ya ubongo wao hii utokana na uvivu,au kukosekanika kwa maarifia,mfano  katika asilimi mia  mwanadamu wa makamo hutumia asilimia tano tu,hii nyingine hubaki bila kutumika ,anza sasa kuutumia ubongo wako ukuuletee mabadiliko,wewe unauwezo mkubwa sana wa kutunza kumbukumbu na kuweza kuletamabadiliko anza leo.

3 comments:

THIS IS YOUR PLACE TO COMMENT