JINSI YA KUWA NA KUMBUKUMBU VIZURI :
Mwaka 2009 nilikuwa mzumbe university nilikuwa katika somo la IT(Information technology)nikapata wazo kama kweli vichwa vetu vingekuwa ni komputa kirahisi tu ningewashauri watu waongeze chip za komputa ili kuongeza kiwango cha kutunza kumbukumbu vichwani(ubongoni) mwao,lakini ubongo wa mwanadamu ni mashine ambayo ipo na mambo chungu nzima kuliko kifaa/mashine yeyote ile ya kisasa,hivyo basi kama mtu anataka kuboresha kumbukumbu kichwani anahitaji juhudi Fulani hivi,chukulia mfano ni kama mtu anayekwenda kufanya mazoezi ya kunyanyua vitu vizito kadri anavyo zidisha na kuweka juhudi ndoo mishipa na misuli yake inavyozidi kutanuka hivyo hivyo katika kuboresha utunzaji wa kumbukumbu inafanya kazi wa kukumbuka unaongezeka kadri unavyofanya mazoezi ya kutunza vizuri kumbukumbu.Kuna aina kadhaa ya vitu vya kutunzia kumbukumbu mfano twasira ya picha,sentensi,mizaha,njia za loc, nk.Zifuatazo ni namna mbalimbali za kuboresha utunzaji wa kumbukumbu vizuri:
1.Mazoezi ya mara kwa mara,husaidia kuongeza oxygen kwenye ubongo ,hivyo kupunguza majanga ambayo hupeleke kutoke kupoteza kumbukumbu mfano wa magonjwa kama kisukari na cardiovascular.
2.Jaribu kuthibiti msongo wa mawazo(stress),Msongo hupelekea kuharibu hippocampus zetu,pia msongo wa mawazo hupelekea kuwa ni vigumu mtu kulifuatilia jambokwa umakini,hapa nashauri kufanya meditation inasaidia kutatua tatizo.
3.Kuwa na tabia ya kulala vema,kulala ni muhimu sana katika kuimarisha utunzaji mzuri wa kumbukumbu ,ulalaji wa chini ya masaa saba unasababisha mtu kushindwa kufuatilia jambo kwa umakini pia ulalaji wa kupitiliza masaa nane mfano mtu kulala masaa tisa husababisha matatizo.
4.Acha tabia ya kuvuta sigara,uvutaji wa sigara huzidisha matatizo katika viungo vyetu ambapo hupelekea mtu kupata magojwa ya mshituko(stroke) na pia kuziba mishipa inayokwenda kupeleka oxygen kwenye ubongo.
5.Kula vizuri na sahihi,tafiti zinaonyesha kuwa kuna aina za vyakula vinavyo saidia kuboresha utunzaji wa kumbukumbu ,mfano matunda,mboga za majani,wanga, nk,vitamin B san asana B6 na B12 mfano spinachi,melon,maharagwe ya soya,matunda ya citrus nk,pia vitamin C and E mfano nyanya za nyekundu,karanga,mbegu,samaki wa maji baridi,na mafuta ya walnut
6.Husiasha viungo vingi ikiwezekana,hata kama wewe unajifunza kwa kutizama soma unachojifunza kwa sauti kile unachotaka kukumbuka,hata kama unaweza kukiwekea katika melodi ya nyimbo ili ukiimbe fanya hivyo,hapo utakuwa umehusisha viungo kama macho,mdomo,mkono nah ii inasaidia sana mambo yakiwa mengi hujui la kufanya nk.
7.Pangilia taarifa zako,jaribu kuandika taarifa zako kwenye kitabu kwa mpangilio wa tarehe na taarifa nyingine muhimu.
8.Penda kuwa muelewa ,achana na tabia ya kukariri anza na kuweka tabia ya kuelewa jambo na kuliweza kulieleze kwa lugha yako mwenyewe.
9.Husisha kile ulichokielewa na kwa kiunganisha na taarifa mpya kwa taarifa ulielewa kabla ili kutengeneza kitu kimoja kikamilifu.
Kulingana na tafiti mbalimbali wanadamu wengi inasemekana hutumia asilimia ndogo sana ya ubongo wao hii utokana na uvivu,au kukosekanika kwa maarifia,mfano katika asilimi mia mwanadamu wa makamo hutumia asilimia tano tu,hii nyingine hubaki bila kutumika ,anza sasa kuutumia ubongo wako ukuuletee mabadiliko,wewe unauwezo mkubwa sana wa kutunza kumbukumbu na kuweza kuletamabadiliko anza leo.
that gud broo
ReplyDeletereal real fine job brother
ReplyDeletewow that real fine
ReplyDelete