Dashboard Builder for Access 2.0 Antivirus Report

Thursday, December 16, 2010

TOO MUCH TALKING......listen twice as talk


KUONGEA SANA  INAWEZA KUKUSABABISHIA WEWE UKOSE  FURSA ZA NAFASI NA MAARIFA KUTOKA KWA WENGINE:
Binadamu ameumbwa  na macho mawili,masikio mawili hii ni viungo muhimu sana katika kumpatia mwanadamu taarifa kutoka kwa wengine,mdomo ni mmoja tu kapatiwa na kutufanya sisi  kutoa taarifa kwa wengine,kwa mantiki ya kawaida hii inamaanisha kuwa wewe  unatakiwa kupokea mara mbili  zaidi ya kile unachokitoa kwa wengine,nahii haina ubishi na haijalishi wewe ni nani au unafanya nini hii ndio sheria iliyo toka enzi na enzi kuanzia china ,ulaya,Afrika na kote duniani wengi watoaji taarifa za kutoka kwao kuliko kupoke huishia kuwa wepesi wa mwili,fikra na kukosa kujiamini kwa mambo yao kwa kuwa hawana jipya au jambo wengine hawalifaamu na kuishia kuwa watu wa kawaida sana na kuwanufaisha wenzao kukua,utaweza jiuliza sana kama ndoo hivyo kwa nini mtu kama mwanasiasa au mchungaji au shehe wanawahuburia sana watu wao lakini kila siku bado wapo imara sana ,sheria ipo pale pale hapa sio kama hawapati taarifa kutoka kwa wengine huwa wanapata sana mfano kupitia kusoma biblia,quruani, novel na vitabu vingine,pia,meditation, kuangalia movies,taarifa za habari hivi  vyote ni vyanzo vya kupata taarifa
Katika maisha  ya kila siku nimeshuhudia  vilio mbalimbali kutoka kwa watu wakijilaumu  na kusema wao si chochote hapa duniani na kweli wenzao hawawathamini  na kamavile wametengwa pasipo  maagano rasmi ya kutopokea taarifa muhimu kutoka kwa wengine,lakini ukiangalia chanzo  cha tatitizo linatokana na wao kuongea sana na kusababisha wao kufukuza maarifa kutoka kwa wengine na taarifa nyingine muhimu .Dunia  hii ndugu imeumbwa na kanuni na jinsi ya kuishi inabidi tutumie kanuni kwa yeyote Yule anayeenda kinyume na kanuni hizi  lazima aangalie wapi alipokosea na arudi nyuma ili asahihishe kosa anza sasa kuwa mjanja kataa taarifa zako kila mtu akazijua hata kama ni mkeo,mzazi au ndugu yako shirikiana nao lakini sio kwa kila taarifa uliyokuwa nao namaanisha kuwa na siri au” msiri” ,binadamu aliyekosa usiri anamatitizo Fulani maana hata mungu ni msiri sana ili shetani kwa wale wanaomaamini asimpiku jaribu kupokea  kutoka kwa wengine  zaidi au soma vitabu sasa,
Njia nyingine ya kutokuwa mzungumzaji sana ni kupenda kuyachukulia mazungumzo  yako ni ya kawaida na sio ya ushindani kwa wengine lengo ni kufikia muafaka. Tatu,unapoona mtu anazungumza acha kumkatisha msubirie mpaka atakapo maliza,na hata kama ataongea sana itafika wakati yeye atatambua wewe pia unahitaji kuongea, hakuna mtu mkamilifua jua hilo.
Mara zote huwa nasema huwa tunafukuza ndoto za kufanikiwa pale  tunapochukua muda wetu kuongea sana kwa kupitiliza anzan sasa kutafuta taarifa muhimu kuliko kutoa ovyo ovyo taarifa  soma  sana vitabu humo ndiko kuna taarifa muhimu,udhuria mikutano muhimu,soma magazine mbalimbali kama fobres magazine kweli utafanikiwa mafanikio ni kwa wote maana dunia  ni yangu na wewe na wengine wote.

Sunday, December 12, 2010

TUNAISHI KWA KUTEGEMEANA ACHA VITA
Dunia sasa imegeuka kijiji ,utandawazi ndoo sera inayoendesha ulimwengu ,mikono yake ipo
kila mahali uanpokuwa ukiwa nje ya kanuni za utandawazi itachukua muda wewe kuendelea,soko
huruia ndoo inaangaza dunia zima kuanzia USA,UK,Tanzania mpaka China na kote duniani,kila mtu
anapigania kuwa na mtandao wa marafiki,business partners wengi kwa wingi pasipo kikomo,wengi
wanapigania kujifunza tamaduni za wengine kwa kasi ili waweze kusurvive katika hii dunia maana
ndoo sera inavyosema.Je ulisha wahi kujiuliza siku ukianzisha au vita unayo sasa kupigana au
kutoelewana na wezako huoni ni kizingiti ndugu yangu,kuna watu wengu katika utafiti wangu mdogo
nimegundua wanashindwa kuendelea kwa kuwa ya kuwa na maadui,kuna mwanamziki wa Uganda
Jose chameleon alisema ameamua kumaliza beef yake na Bebe cool kwa kuwa ina msababishia
kukosa deal kubwa za kuimba nje ya nchi na pia ndani ya nchi,hii ilikuwa yu sababu ya kuacha beef na
siyo sababu nyingine.Ndugu yangu dunia ilivyo kutokea kipindi kilichopita ni katika mtizamo wa huyu
kashinda na huyu kashindwa(win loose) na kweli mtizamo huu sio mzuri na ndoo unasababisha vita na
mtafaruku katika jamii na ndoo huu unasababisha vita tokea enzi na enzi hapa duniani lakini mimi na
wezangu baadhi ya waandishi tunasema hapana sasa ni yatosha tuanze kuishi win win sides(pande zote
zote zimesinda)hakuna aliyeshinda,nilibahatika kuangalia mashindano fulani ya mziki baadaya
kutangazwa mshindi ndipo ugomvi kupitia wasanii ukafumuka nikagundua win loose imewaathiri,hata
sasa sera ya dunia ndoo inavyosema hivyo juzi tulikuwa na uchaguzi hapa Tanzania,upande wa
zanzibar baada ya DR Shein kutangazwa mshindi Mpinzani wake Maalim Seif alisema sote
tumeshinda,wewe leo unangania uitwe mshindi yule aitwe kashindwa baada ya hapo kweli utakuwa
na amani kichwani ukifikiria adui wako?Ndugu yangu kila mwandamu anhitaji kuungwa mkono na
kupewa matumaini na mtu mwingine,chukulia wewe ni mfanya biashara unahitaji wateja wa bidhaa
zako huwezi kupata kipato kama huna wateja,je embu jiulize kama una adui wengi huoni kama ni
kizingiti katika kuogeze kipato kwako?tena inakuwa mbaya ukianzisha vita halafu huna jeshi hapa
ndugu yangu ni mbaya sana watu kumaliza kwa kubomoa misingi ya kazi yako na kufika
tamati(mwisho)pasipo kujijua na kuanza kutapatapa,Martin Luther king anasema kama huwezi
kupigana na sisi basi jiunge na sisi.Sasa ni jinsi gani ya kuungwa mkono na wengine haitaji kutumia
nguvu ili watu wakukubali njia rahisi na yenye tija ni kuwajali,kuwaheshimu na kuwathamini watu
haijalishi ni nani,kitaalamu haijalishi ni wapi anatokea Afrika,ulaya au wapi binadamu yeyote anahitaji
kupendwa na anahitaji kuona yeye wa thamani.
Zifuatazo ni njia unazoweza kutumia kuonyesha una wathamin binadamu wengine:
1.Penda kuwasalimia watu kwa vifupi vya hadhi ya majina yao mfano Mr,Mrs,Miss,Dr,Prof,Sir na
kadhalika ,wasalimu kinyenye kevu na kibusara
2.Mara zote tumezungukwa na dunia iliyo na watu wasio wakamilifu mfano kuna maneno ya
umbea,wivu,uongo sehemu tunamofanya kazi,ishi na kadhalika ndugu yangu kama huwezi kuonge
chochote kizuri au jambo jema kuhusu mtu fulani bora unyamaze kimya.
3.Usujaribu kuwapinga wengine pasipo kuwapa jibu mbadala au njia mbadala iliyo bora ,wapinge
watu katika kuwajenga
4.Mabadiliko yanaanzia kwako na kusambaa kwa wengine, anza sasa kufanya mazoezi ya
kuwathamini wengine anzia kwa mkeo,watoto wako,familia yako,marafiki wako,jirani zako,jamii kwa
ujumla....
5.Wafanye wengine wahisi kuwa wa muhimu sana na hii inakuja kwa kuwaambia kuwa una
wapenda ,unawajali na wao ni watu muhimu sana katika maisha yako nk
Ndugu yangu sisi hapa duniani tupo tofauti wenye mitizamo tofauti na inawezekana sawa ,na wakati
mwingine tupo kwa kazi zinzofanana hata kama ni hivi usichulie ni adui wako bali ni mwezako katika
kukamilisha maono yako.