Dashboard Builder for Access 2.0 Antivirus Report

Sunday, December 12, 2010

TUNAISHI KWA KUTEGEMEANA ACHA VITA
Dunia sasa imegeuka kijiji ,utandawazi ndoo sera inayoendesha ulimwengu ,mikono yake ipo
kila mahali uanpokuwa ukiwa nje ya kanuni za utandawazi itachukua muda wewe kuendelea,soko
huruia ndoo inaangaza dunia zima kuanzia USA,UK,Tanzania mpaka China na kote duniani,kila mtu
anapigania kuwa na mtandao wa marafiki,business partners wengi kwa wingi pasipo kikomo,wengi
wanapigania kujifunza tamaduni za wengine kwa kasi ili waweze kusurvive katika hii dunia maana
ndoo sera inavyosema.Je ulisha wahi kujiuliza siku ukianzisha au vita unayo sasa kupigana au
kutoelewana na wezako huoni ni kizingiti ndugu yangu,kuna watu wengu katika utafiti wangu mdogo
nimegundua wanashindwa kuendelea kwa kuwa ya kuwa na maadui,kuna mwanamziki wa Uganda
Jose chameleon alisema ameamua kumaliza beef yake na Bebe cool kwa kuwa ina msababishia
kukosa deal kubwa za kuimba nje ya nchi na pia ndani ya nchi,hii ilikuwa yu sababu ya kuacha beef na
siyo sababu nyingine.Ndugu yangu dunia ilivyo kutokea kipindi kilichopita ni katika mtizamo wa huyu
kashinda na huyu kashindwa(win loose) na kweli mtizamo huu sio mzuri na ndoo unasababisha vita na
mtafaruku katika jamii na ndoo huu unasababisha vita tokea enzi na enzi hapa duniani lakini mimi na
wezangu baadhi ya waandishi tunasema hapana sasa ni yatosha tuanze kuishi win win sides(pande zote
zote zimesinda)hakuna aliyeshinda,nilibahatika kuangalia mashindano fulani ya mziki baadaya
kutangazwa mshindi ndipo ugomvi kupitia wasanii ukafumuka nikagundua win loose imewaathiri,hata
sasa sera ya dunia ndoo inavyosema hivyo juzi tulikuwa na uchaguzi hapa Tanzania,upande wa
zanzibar baada ya DR Shein kutangazwa mshindi Mpinzani wake Maalim Seif alisema sote
tumeshinda,wewe leo unangania uitwe mshindi yule aitwe kashindwa baada ya hapo kweli utakuwa
na amani kichwani ukifikiria adui wako?Ndugu yangu kila mwandamu anhitaji kuungwa mkono na
kupewa matumaini na mtu mwingine,chukulia wewe ni mfanya biashara unahitaji wateja wa bidhaa
zako huwezi kupata kipato kama huna wateja,je embu jiulize kama una adui wengi huoni kama ni
kizingiti katika kuogeze kipato kwako?tena inakuwa mbaya ukianzisha vita halafu huna jeshi hapa
ndugu yangu ni mbaya sana watu kumaliza kwa kubomoa misingi ya kazi yako na kufika
tamati(mwisho)pasipo kujijua na kuanza kutapatapa,Martin Luther king anasema kama huwezi
kupigana na sisi basi jiunge na sisi.Sasa ni jinsi gani ya kuungwa mkono na wengine haitaji kutumia
nguvu ili watu wakukubali njia rahisi na yenye tija ni kuwajali,kuwaheshimu na kuwathamini watu
haijalishi ni nani,kitaalamu haijalishi ni wapi anatokea Afrika,ulaya au wapi binadamu yeyote anahitaji
kupendwa na anahitaji kuona yeye wa thamani.
Zifuatazo ni njia unazoweza kutumia kuonyesha una wathamin binadamu wengine:
1.Penda kuwasalimia watu kwa vifupi vya hadhi ya majina yao mfano Mr,Mrs,Miss,Dr,Prof,Sir na
kadhalika ,wasalimu kinyenye kevu na kibusara
2.Mara zote tumezungukwa na dunia iliyo na watu wasio wakamilifu mfano kuna maneno ya
umbea,wivu,uongo sehemu tunamofanya kazi,ishi na kadhalika ndugu yangu kama huwezi kuonge
chochote kizuri au jambo jema kuhusu mtu fulani bora unyamaze kimya.
3.Usujaribu kuwapinga wengine pasipo kuwapa jibu mbadala au njia mbadala iliyo bora ,wapinge
watu katika kuwajenga
4.Mabadiliko yanaanzia kwako na kusambaa kwa wengine, anza sasa kufanya mazoezi ya
kuwathamini wengine anzia kwa mkeo,watoto wako,familia yako,marafiki wako,jirani zako,jamii kwa
ujumla....
5.Wafanye wengine wahisi kuwa wa muhimu sana na hii inakuja kwa kuwaambia kuwa una
wapenda ,unawajali na wao ni watu muhimu sana katika maisha yako nk
Ndugu yangu sisi hapa duniani tupo tofauti wenye mitizamo tofauti na inawezekana sawa ,na wakati
mwingine tupo kwa kazi zinzofanana hata kama ni hivi usichulie ni adui wako bali ni mwezako katika
kukamilisha maono yako.

No comments:

Post a Comment

THIS IS YOUR PLACE TO COMMENT