Dashboard Builder for Access 2.0 Antivirus Report

Saturday, December 4, 2010

salamu za Kilawe

KUONGEA SANA  INAWEZA KUKUSABABISHIA WEWE UKOSE  FURSA ZA NAFASI NA MAARIFA KUTOKA KWA WENGINE:
Binadamu ameumbwa  na macho mawili,masikio mawili hii ni viungo muhimu sana katika kumpatia mwanadamu taarifa kutoka kwa wengine,mdomo ni mmoja tu kapatiwa na kutufanya sisi  kutoa taarifa kwa wengine,kwa mantiki ya kawaida hii inamaanisha kuwa wewe  unatakiwa kupokea mara mbili  zaidi ya kile unachokitoa kwa wengine,nahii haina ubishi na haijalishi wewe ni nani au unafanya nini hii ndio sheria iliyo toka enzi na enzi kuanzia china ,ulaya,Afrika na kote duniani wengi watoaji taarifa za kutoka kwao kuliko kupoke huishia kuwa wepesi wa mwili,fikra na kukosa kujiamini kwa mambo yao kwa kuwa hawana jipya au jambo wengine hawalifaamu na kuishia kuwa watu wa kawaida sana na kuwanufaisha wenzao kukua,utaweza jiuliza sana kama ndoo hivyo kwa nini mtu kama mwanasiasa au mchungaji au shehe wanawahuburia sana watu wao lakini kila siku bado wapo imara sana ,sheria ipo pale pale hapa sio kama hawapati taarifa kutoka kwa wengine huwa wanapata sana mfano kupitia kusoma biblia,quruani, novel na vitabu vingine,pia,meditation, kuangalia movies,taarifa za habari hivi  vyote ni vyanzo vya kupata taarifa
Katika maisha  ya kila siku nimeshuhudia  vilio mbalimbali kutoka kwa watu wakijilaumu  na kusema wao si chochote hapa duniani na kweli wenzao hawawathamini  na kamavile wametengwa pasipo  maagano rasmi ya kutopokea taarifa muhimu kutoka kwa wengine,lakini ukiangalia chanzo  cha tatitizo linatokana na wao kuongea sana na kusababisha wao kufukuza maarifa kutoka kwa wengine na taarifa nyingine muhimu .Dunia  hii ndugu imeumbwa na kanuni na jinsi ya kuishi inabidi tutumie kanuni kwa yeyote Yule anayeenda kinyume na kanuni hizi  lazima aangalie wapi alipokosea na arudi nyuma ili asahihishe kosa anza sasa kuwa mjanja kataa taarifa zako kila mtu akazijua hata kama ni mkeo,mzazi au ndugu yako shirikiana nao lakini sio kwa kila taarifa uliyokuwa nao namaanisha kuwa na siri au” msiri” ,binadamu aliyekosa usiri anamatitizo Fulani maana hata mungu ni msiri sana ili shetani kwa wale wanaomaamini asimpiku jaribu kupokea  kutokakwa  zaidi au soma vitabu sasa,
Njia nyingine ya kutokuwa mzungumzaji sana ni kupenda kuyachukulia mazungumzo  yako ni ya kawaida na sio ya ushindani kwa wengine lengo ni kufikia muafaka. Tatu,unapoona mtu anazungumza acha kumkatisha msubirie mpaka atakapo maliza,na hata kama ataongea sana itafika wakati yeye atatambua wewe pia unahitaji kuongea, hakuna mtu mkamilifua jua hilo.
Mara zote huwa nasema huwa tunafukuza ndoto za kufanikiwa pale  tunapochukua muda wetu kuongea sana kwa kupitiliza anzan sasa kutafuta taarifa muhimu kuliko kutoa ovyo ovyo taarifa  soma  sana vitabu humo ndiko kuna taarifa muhimu,udhuria mikutano muhimu,soma magazine mbalimbali kama fobres magazine kweli utafanikiwa mafanikio ni kwa wote maana dunia  ni yangu na wewe na wengine wote.

No comments:

Post a Comment

THIS IS YOUR PLACE TO COMMENT