d KUWA MSHINDI KATIKA KULALA VEMA:
Baada ya kazi na miangaiko mingi ya siku mara ofisini,nyumbani na sehemu nyingine mchoko kama huu wote huishia kitandani lakini mara nyingi watu wengi huwa wanalalamika mara usingizi sipati ,hata muda mwingine wengine hupata usingizi asubuhi hili tatizo limekuwa kubwa siku hadi siku ndani ya jamii zetu, kitaalamu tatizo la kukosa usingizi huitwa insomnia ,na mara nyingi wengi wanaokumbwa na tatizo hili wamekuwa wakijaribu kutafuta suluhu mbalimbali mathalani wengi wanajaribu kutumia madawa ili tu waweze kulitibu tatizo lakini mara zote hii inakuwa suluhu ya muda mfupi tu,siku moja nilikuwa na dada mmoja alikuwa ananilalamikia kuwa yeye hapati usingizi nahivi sasa yapata miezi sita.kweli ilinigusa sana na pia aliniambia amejaribu kutumia madawa lakini hayakufua dau kweli hii ni kama kifungo mtu yupo nilimapatia ushauri na baadanya muda aliniambia tatizo limekwisha,katika tafiti mbalimbali mathalani kutoka university of Harvard medical school wanasema kulala ni muhimu sana kwa afya ya mwanadamu muda wakawaida wa mwanadamu kulala kwa usingizi wa afya njema ni masaa manane,utafiti unaonyesha kuwa watu wanaolala kupitiliza masaa nane mfano wanaolal masaa tisa,kumi nakathalika huwa wanajitafutia matatizo,inasemekana watu hawa kiwango cha waokuishi ni kidogo sana maana ni rahisi kushambuliwa na magonjwa ya moyo mfano heart stroke na mengine kuliko watu wanaolala masaa ya kawaida nane,miongoni mwa wanaolala masaa tisa kiwango cha kufa ni asilimia286 juu zaidi ya wanaolala masaa saba,vilevile wanaolala masaa chini ya nane mfano matano hukumbwa na matatizo kama kuhisi maumivu kutwa nzima,kutojisikia vema (discomfort) na kwa ujumula huishia kuthoofika kiafy.
Kuna jinsi yakufanya ili uweze kupata usingi murua na mzuri ,tafiti zinaonyesha mambo yafuatayo yanaweza kukusaidia kuwa na usingizi mzuri kabla ya kwenda kitandani:
i)Penda fanya mazoezi mepesi kabla ya kwenda kulala,mathalani kunyoosha viungo,puishapu kadhaa
ii)Oga na maji ya vuguvugu kabla ya kwenda kulala nyakati za usiku.
iii)Sikiliza mziki taratibu na wenye kukuliwaza,ni muhimu sana kununua cd za muziki wa taratibu wakati wa usiku unaiweka na kusikiliza
iv)usipende kwenda kulala wakati huohuo umetoka kula chakula,usipende kuingia kitandani na tumbo lililojaa chakula havita kuletea usingizi
v)Matatizo yako ya siku nzima usiende nayo kitandani
vi)Kaa katika mawazo mazuri,furaha,amani ya moyo
vii)jiachie mwili wako,akili yako,weka hisia wewe ni mwepesi,weka fikra kuwa usingizi unakuja na jiweke katika mazingira ya kuukubali usingizi
No comments:
Post a Comment
THIS IS YOUR PLACE TO COMMENT