Dashboard Builder for Access 2.0 Antivirus Report

Monday, March 14, 2011

Aina ya biashara waweza anziasha kwa mafanikio

AINA YA BIASHARA WAWEZA ANZISHA KWA MAFANIKIO MAKUBWA

 
Biashara na dunia
ya digitali yahitaji mengi maarifa  ya
kuwekeza ili  kukubakisha katika mfumo
,nimeshuhudia mamia ya watu wakirudi katika umasikini ulio kidhiri  lakini hapo awali walikuwa na  biashara kubwa tu za maana,dunia ya sasa
yahitaji kufikiri kwa haraka ili ufanye maamuzi sahihi ndani ya muda mfupi,kama
ukikosea  kufikiri vema mfumo  unakutupa nje,Biashara ya karne hii zipo za
aina mbili bidhaa na kutoa huduma,hizi zote zinahitaji uwekezaji mkubwa wa
maarifa ,huduma huhitaji  mtaji mdogo
sana wa maarifa na huwa inalipa kwa kiasi kikubwa ,mathalani  idadi kubwa wa matajiri duniani  hutokea kwa huduma mfano  Helu slim,Bill gates Michael dell na wengi
sana ni huduma,japo bidhaa inalipa sana sema inahitaji kuwekaza  zaidi kuliko huduma pia zote huduma na bidhaa zinahitaji mtu awe na malengo ili uweze
kudumu,katika ukanda wa afrika mashariki kuna aina mbalimbali zinazoendeshwa  lakini swali kuu
ni je hizi biashara huwa zinadumu baada ya miaka mitatu au zinakufa?kabla ya
kujengwa kwa  mlimani city barabara ya
sam nujoma na kutoka mwenge kwenda posta kulikuwa na maduka na baa nyingi je
leo ukipita zipo?mara nyingi biashara nyingi huanzishwa pasipo  malengo,dira na maono kamili nyingi hutokea
kwa sababu Fulani kafanikiwa  basi mwingine
huenda kuwekeza sekta hiyo ,katika dunia ya sasa kuna aina zifuatazo kuu za
biashara:



   (i)Biashara ya asili(traditional business)
hii ni biashara ambayo imezoeleka miongoni
mwa wengi sana sana wazawa,katika hii mtu anakuwa na mtaji na kufungua biashara
yake baada ya kufuata mlolongo wa kuandikisha biashara yake,mfano wa hizi
biashara ni  baa,biashara ya daladala
nchini,biashara ya maduka,nk.Hii aina ya biashara ni maarufu sana miongoni mwa
wanajamii ,mara nyingi ipo sana sana ipo maeneo ya wanapotokea watu wa tabaka la
tatu na la pili,hapa ndipo kwenye walipa kodi wengi ukiachilia mbali
wafanyakazi.Sifa kubwa yah ii aina ni ina aina ya usambazaji wa mlolongo kutoka
kiwandani,kwenda kwa wauzaji wa jumla,rejareja na hatimaye mtumiaji.



 (ii)Biashara kutumia jina la kampuni kubwa duniani kibiashara(franchises),
makapuni mengi hapa nchini ni yakununua brand name
ya kampuni kubwa ya nje na kulitumia katika biashara baada ya kukidhizi viwango
vya kampuni husika,mfano Tanzania kuna kampuni za cocacola,steers restaurant,mc
Donald,the guardnian,dasani,daily news,ITV, nk hizi zote zimenunua  majina ya hizi kampuni baada ya kufikia viwango vya kampuni husika,sifa kubwa
ya hizi biashara unatakiwa uwe na mtaji mkubwa maana unatakiwa ulipe kodi
(loyality)kwa kampuni mama au kwa lugha ,uchangie gharama za matangazo kwa
kueneza kwa gharama yako haya matangazo kutoka nje na jina nzuri(goodwill).Pia
siku hizi kampuni nyingi zinafanya kujisajili kwa kampuni kubwa(affiliation) .



(iii)Biashara za mitandao(networking market)
,hii ni ndoo biashara iliyoibuka miaka ya
sasa hivi Afrika ,japo ilikuwepo toka miaka ya 1940’s maeneo ya nchi za
magharibi ,wanazuoni wengi  wametabiri
ndio biashara ya karne hii baada ya kuondoa zile gharama za utangazaji katika
ya mzalishaji na mtumiaji,hapa inakuwa muuzaji ndio mteja na kadri anavyoleta wateja wengine analipwa  kulingana na idadi na hiyo idadi ikileta
wateja wengine hawa wote watahesabika ni Yule wa kwanza ,na wale waliwaleta
wengine watalipwa kwa hiyo idadi,mfano A ameleta  B ,C,na D basi A atalipwa kwa gharama za
matangazo za kuwaleta B,C na D maana hii itatumika kama vocha ya A kulipwa
,mathalani  B,C na D wakaleta wengine
E,G,H,I,J,K  hapa A  atalipwa kwa gharama za wote hawa kupitia
vocha za B,C na D,na pia B,C na D watalipwa kwa vocha za E,G,H,I,J,k nao hivyo
hivyo kwa hawa kama wakileta watu na kuwa wateja na wauzaji huu wote ni mtandao
unakuwa na kusonga mbele sifa kuu wale waliowahi ndio watanufaika sana.



            Biashara za kileo zahitaji ubunifu,na
maarifa mengi hivyo umakini wa kuchagua wapi uangukie unatakiwa umakini sana,biashara
za mitandao ni nzuri sana, kwani kadri mnavyokuwa wengi kunufaika  na kuzidi kuimarika  hivyo kuwa biashara ya kileo.











 

No comments:

Post a Comment

THIS IS YOUR PLACE TO COMMENT