Dashboard Builder for Access 2.0 Antivirus Report

Sunday, December 5, 2010

                   CHUKUA VILIVYO VYAKO HAPA ULIMWENGUNI:
Sayari zipo takribani zaidi ya kumi,japo utafiti bado unaendelea ili kugundua sayari nyingine hapa  ulimwenguni,waweza jiuliza ulimwengu nini?bila shaka kama ni mfuatiliajimzuri wa mambo jibu litakupa ni  muunganiko wa vitu vyote ambavyo ni sayari ambapo ndani yake kuna sayari ya dunia,vitu vingine  vinavyokamilisha neno ulimwengu ni mwezi,nyota,jua  na vingine ambavyo bado kisayansi havijagunduliwa,kila moja  kimoja kinautofauti wake  kutoka kwa kingine,ndani ya sayari ya dunia kuna mengi  kama  milima,mabonde,bahari,wanyama,mimea, binadamu  na viumbe isivyo hai ,lakini cha kushangaza  kila  kitu kipo tofauti na kingine  ukiangalia kwa makini utakuta milima imetofautiana na wanyama,wanyama  wametofautiana na  binadamu yaani kila kimoja kina nafasi yake  na maana yake  yakuwepo hapa kwenye hii sayari ya dunia,katika tafiti na  misemo ya watu mbambali  binadamu  pia wote wametofautiana  maana yake   kila binadamu anajinsi ya tofauti alivyoumbwa kutoka kwa mwingine ,na ndoo maana haijawahi kutokea hata siku moja duniani binadamu wote wakakubaliana  japo kwa sekunde moja dunia nzima na sidhani  kuna siku itatokea,japo kuwa kuna watu mbalimbali wanaoishi ilimradi wamridhishe   au kuna watu wanaoishi kwa kuigana  hii ni katka ulimwengu huu tunaoishi wa” material world” ambapo namba ya material  people inaongezaka  huku namba ya immaterial people inapungua ,lakini turudi hapa,kwanini nasema binadamuwote  tumetofautiana?je kuna siku ulisha wahi  jiuliza natambua mwanadamu mwezangu kwa sura an umbo la mwili wake lilivyo au kwa roho?kama jibu ni kwa roho basi kila mwanadamu ni tofauti  kutoka kwa mwingine,na kila mwanadamu ananafasi sawa kama ilvyo kwa wengine,hakuna mwanadamu aliyemzidi mwingine nikimaanisha kuwa wanadamu wote ni werevu sawa na wajinga sawa mbele za Mungu au hakuna mwanadamu anambania mwenzake asifanikiwe maishani bali ni yeye mwenyewe ana uwezo huo kuamua kufanikiwa au asifanikiwe,hapa wengi hutumia mwili kuamua kufanikiwa wakati wao sio mwili bali wapo katika formless ndugu yangu ili uweze kuwasiliana na wewe inabidi uwe katika umbo lako la formless njia ambazo zinaweza kupeleka katika hali yako ni meditation,sala zaukimya,kutafakari kwa ukimya maeneo mbali na wanadamu,Umbo la mwanadamu ni  vazi tu mwanadamu alipewa ili afurahie maisha ya hapa sayarini achana na nguo wanadamu walizojitengenezeawao wenyewe zinahistoria yake hizi na chimbuko lake.Ndugu yangu ulishawahi jiuliza kuwa sasa kama wanadamu wote ni sawa hasa mbona wengine matajiri na wengine ni masikini?nadhani ni swali linalotekenya kichwa ,ni kweli   napenda kusema hivi dunia iliumbwa kwa principle na  hivyo kama unataka ufanikiwe uwe na furaha ,fedha,kuungwa mkono,kushinda majaribu yote  kuna kanuni  inabidi ufuate ili uweze fanikiwa katika hayo,ndoo maana unaona kati ya matajiri na masikini wa fedha  tofauti ni mambo wanayoyajua na sii kingine ,kanuni za kuwa tajiri zipo wazi,inaaminika wengi masikini wa fedha pia ni masikini wa mawazo ndoo maana wengi wanakata tama kabla hata hawajaweka  nia mioyoni mwao,wengi wanahusishwa na uvivu wa kufikiri kwa angalau siku moja kwa wiki,kumeditate,kusali kwa ukimya   wengi wao wanapenda vitu ambayo tayari vimetaarishwa mathalani kutizama luninga tamthilia Fulani na vipindi kedede  muda wote,kupiga stori san asana kusikiliza kutoka kwa wengine,kucheza tu michezo mbalimbali  muda wote na kadhalika.Haina haja ya wewe sasa kuanza kumuone mwezako wivu kisa kaendelea yule ni Yule na wewe ni wewe hajakushika mashati akuzuie usifanikiwe wala hajachuma mali zako zile ni zake,kila mwanadamu anautajiri mkubwa wa mali  zilizoangukia upande wale ila wanadamu wanashindwa kuzichuma hizo mali .kuwa tajiri ni kanuni haijalishi wewe ni mdhambi au la,bali inajalisha wewe unazifuata kanuni au la ,sio kipimocha  wewe unasali eti sana hii ni  hapana.
Ndugu yangu kama nilivyosema awali wewe upo katika hali ya formless(roho),ukitaka kujua wewe ni nani inabidi uwepo kitika hali yakonjia  ambazo zinaweza kukufikisha hapo ,meditation ni chaguo bora zaidi,sala za ukimya pia ni nzuri,ukishafika katika hali ya  roho sasa anza kujiuliza wewe nini Mungu kaweka nini ndani yako(kipawa) na pia unataka nini katika hii sayari?,jaribu kudadisi kwa makini na taratibu  tizama mfano katika hawa wote  unataka uwe nani,Msanii,Billionea,Mkuu wa nchi,Kiongozi wa dini,Mfanyakazi,Mwanasayansi,Generali wa jeshi,Mtawala katika mamlaka za serikali na organazesheni zake,Msomi, Mwenyekiti mtendaji wa makampuni makubwa,nakadhalika.Hapa ni wakati mgumu  sana kujua wewe ni nani,lakini yakupasa kufuata sauti iliyokuwa inatoka nafsini mwako sio unachoona kwa wengine,tafuta wewe ni nani?taratibu fuata kinachotoka kwako wewe,baada yaw ewe kujitambua sasa anza sasa kukifanyia kazi kile ambacho umekipata hata kam watu watakukatisha tama,njia iliyo bora ni kungangania jambo kama unauhakika nalo haijalishi  ni changamoto zipi unazipata maana wanaokupa changamoto hawana maono wewe ndoo mwenye maono sasa inakuwaje asiyekuwa na maono  na asiyejua jambo kwa nini akuyumbishe?,ndugu yangu ,anza kutafuta ushauri kwa wataalamu wa hilo jambo lakini kuwa makini watu sio usijaribu kutoa wazo lako  wewe taka ushauri binadamu mara nyingi sio waaminifu ,kisha utafanikiwa katika hilo jambo ukiongezeo asilimia kubwa ya nguvu zako,
Siri kuwa duniani kuna mambo mengi sana  chukua yaliyo yako tu na ondoka zako,huu ulimwengu  umejaa mengi makelele  yanachafua hii dunia,wengi wanasema wanavyosema jiulize wewe unasemaje?acha kuiga watu kila mtu ana namna ya kufanikiwa,jiulize kama utaiga ukifika kwa wale wakatishaji tama si utashindwa tu jiamini ndugu yangu.Dunia imejengwa na Mungu kwa misingi ya kanuni na kufanikiwa ni kanuni.Zingatia hili usipende kuropoka ovyo ovyo malengo yako kwa  watu wengi ni waaribu maono ngangania na kile unachokijua ndugu yangu.
                                                                

No comments:

Post a Comment

THIS IS YOUR PLACE TO COMMENT