KUWA MUWAZI MOJA KWA MOJA BADO NI SERA NZURI
Tabia na utamaduni ni vitu vinyoweza kumjulisha mtu mmoja kwa wengine kwamba yeye ni nani ,mathalani yeye mambo haya hayapendi na mambo haya anayapenda,lengo la watu wengi ni kuwa na amani ya moyo,je ulishawahi jiuliza siku unawezaje kuipata amani wakati wewe haueleweki kama upo kwa upande gani?ili watu waajue jinsi gani ya kuishi nawe inabidi uwNo table of figures entries found.e wazi ilibaadae isije kuja matatizo baadae,mara nyingi sera ya mtu kuwa straight yaani kukiri moja kwa moja kama ni nyeusi au nyeupe imekuwa ni shida sana hapa kwetu Africa na inachukua muda sana watu kuifanyia kazi, hii mara nyingi inatokana na hofu ya kuogopa wanadamu wengine alisema Beatrice Nyamburua kutoka Nairobi ,utakuta mtu mnapanga naye maagano ya jambo Fulani badala ya yeye kukataa moja kwa moja ananyamaza kimya halafu mwisho wa siku anakuja kukuambia kuwa jambo hilo haliwezekani hii kweli inauma sana pia kisaikolojia ina muathiri Yule unaye mgeuka,pia katika Nyanja ya dini kwa wale waamini ni dhambi kumpotezea mtu muda wake kwa uzembe wako wa kushindwa kujua kuwa muwazi moja kwa moja ndoo jawabu ya jambo ulilofanya.Nilikuwa ofisi moja pale Kenya nafanya kazi ,msaidi wa bosi wa kampuni yetu alikuwa anashauri bosi mambo mbalimbali kutokana na ofu ya kuogopa akimshauri bosi wake kinyume na bosi wake anavyofikir bosi angemropokea na hata kumfukuza kazi hivyo anajifanya kuwa yupo mstari wa mbele kumsapoti bosi wake kwa mambo yote mabaya na mazuri badala ya kutoa ushauri unaofaa na kuishia kumpotosha kisa anahofia akisema itakavyo atapoteza ajira yake,alafu ikitokea watu wakaanza kumpa changamoto bosi wake ghafla akamgeuka bosi anajifanya kumponda bosi wake na kumchafulia jina lake kuwa bosi wake ni mbishi,anangania mawazo yake tu mara bosi vile wakati wa vikao vyote yeye alikuwa anitikia ndio siku mambo yapoanza kwenda kombo yeye anaanza kugeuka bosi wake si uungwana kabisa na uzandiki wa hali ya juu maaana haiwezekani make vikao na katika mchakato wote mpo pamoja na ulikuwa kimya na kukubaliana sawa mwishoe unakuja kumkana.Nimekuwa nikifuatilia chimbuko la jambo hili hapa kwetu afrika nah ii kweli naamini inatokana na kutokuwa huru kwa watu na kuwa na hofu juu ya maisha yaani kwa lugha nyepesi ni kuwa watumwa wa wanadamu wezeko,japokuwa kuna sababu nyingine ambayo ni muhimu na ndoo chimbuko,kuwa viongozi wetu wa awali walipanda mbegu hii na sisi ndoo matunda ya hiyo mbegu iliyopandwa na viongozi wetu wa mwazo,ukisikate taama ukisia hayo kama walipanda mbegu hiyo basin a sisi tupande mbegu nyingine iliyo nzuri kwa taifa la leo na kesho,kuwa muwazi sasa kwa lolote lile,sema ndio au hapana,Ndugu yangu yangu katika hii dunia kama unataka kuishi kwa furaha jaribu kuwa muwazi moja kwa moja kweli utakuwa na amani na furaha usiogope hamna mtu kashikilia hatma ya maisha yako ni wewe pekeehuwezi kujua ni kiasi gani cha maumivu una msababishia Yule unaye muongopea.
Tujifunze jinsi ya kumaliza kiini cha tatizo ,tuache kupanda mbegu ya uongo katika familia zetu ,wazazi wetu walituongopea kuwa watoto wananuliwa hopitali je unaona huu uongo ni wa kuendelea nao kizazi hadi kizazi?ni muda wa kuwa wa kweli sio waongo huku twajua kweli ni upi…,je ushawahi kuhisi siku kama mwezi mmoja ukaishi kwa ukweli na sio longolongo,alafu mwezi ukaishi kwa longolongo na uongo ni upi mwezi ambao unefanikiwa amani ya moyo?ni kazi ndogo tu sisi kuruhu hali ya kubadilika ndani ya nafsi zetu nasi tutakuwa watu wema na wenye amani kubwa.
No comments:
Post a Comment
THIS IS YOUR PLACE TO COMMENT