KUONGEA SANA INAWEZA KUKUSABABISHIA WEWE UKOSE FURSA ZA NAFASI NA MAARIFA KUTOKA KWA WENGINE:
Binadamu ameumbwa na macho mawili,masikio mawili hii ni viungo muhimu sana katika kumpatia mwanadamu taarifa kutoka kwa wengine,mdomo ni mmoja tu kapatiwa na kutufanya sisi kutoa taarifa kwa wengine,kwa mantiki ya kawaida hii inamaanisha kuwa wewe unatakiwa kupokea mara mbili zaidi ya kile unachokitoa kwa wengine,nahii haina ubishi na haijalishi wewe ni nani au unafanya nini hii ndio sheria iliyo toka enzi na enzi kuanzia china ,ulaya,Afrika na kote duniani wengi watoaji taarifa za kutoka kwao kuliko kupoke huishia kuwa wepesi wa mwili,fikra na kukosa kujiamini kwa mambo yao kwa kuwa hawana jipya au jambo wengine hawalifaamu na kuishia kuwa watu wa kawaida sana na kuwanufaisha wenzao kukua,utaweza jiuliza sana kama ndoo hivyo kwa nini mtu kama mwanasiasa au mchungaji au shehe wanawahuburia sana watu wao lakini kila siku bado wapo imara sana ,sheria ipo pale pale hapa sio kama hawapati taarifa kutoka kwa wengine huwa wanapata sana mfano kupitia kusoma biblia,quruani, novel na vitabu vingine,pia,meditation, kuangalia movies,taarifa za habari hivi vyote ni vyanzo vya kupata taarifa
Katika maisha ya kila siku nimeshuhudia vilio mbalimbali kutoka kwa watu wakijilaumu na kusema wao si chochote hapa duniani na kweli wenzao hawawathamini na kamavile wametengwa pasipo maagano rasmi ya kutopokea taarifa muhimu kutoka kwa wengine,lakini ukiangalia chanzo cha tatitizo linatokana na wao kuongea sana na kusababisha wao kufukuza maarifa kutoka kwa wengine na taarifa nyingine muhimu .Dunia hii ndugu imeumbwa na kanuni na jinsi ya kuishi inabidi tutumie kanuni kwa yeyote Yule anayeenda kinyume na kanuni hizi lazima aangalie wapi alipokosea na arudi nyuma ili asahihishe kosa anza sasa kuwa mjanja kataa taarifa zako kila mtu akazijua hata kama ni mkeo,mzazi au ndugu yako shirikiana nao lakini sio kwa kila taarifa uliyokuwa nao namaanisha kuwa na siri au” msiri” ,binadamu aliyekosa usiri anamatitizo Fulani maana hata mungu ni msiri sana ili shetani kwa wale wanaomaamini asimpiku jaribu kupokea kutoka kwa wengine zaidi au soma vitabu sasa,
Njia nyingine ya kutokuwa mzungumzaji sana ni kupenda kuyachukulia mazungumzo yako ni ya kawaida na sio ya ushindani kwa wengine lengo ni kufikia muafaka. Tatu,unapoona mtu anazungumza acha kumkatisha msubirie mpaka atakapo maliza,na hata kama ataongea sana itafika wakati yeye atatambua wewe pia unahitaji kuongea, hakuna mtu mkamilifua jua hilo .
Mara zote huwa nasema huwa tunafukuza ndoto za kufanikiwa pale tunapochukua muda wetu kuongea sana kwa kupitiliza anzan sasa kutafuta taarifa muhimu kuliko kutoa ovyo ovyo taarifa soma sana vitabu humo ndiko kuna taarifa muhimu,udhuria mikutano muhimu,soma magazine mbalimbali kama fobres magazine kweli utafanikiwa mafanikio ni kwa wote maana dunia ni yangu na wewe na wengine wote.
yabidi ku cool
ReplyDeletekool
ReplyDelete